Msimuliaji : Dokta. mungu wa kabili …….0744 000 473
Asalaam Aleykum Ndugu zanguni. Habari za mwaka mpya wa 2017.
Ni matumaini yangu kuwa Mwenyezi Mungu amewavusha salama.
Niende kwenye mada ya leo, Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipata kesi za watu ambao nikiwatazama katika jicho la rohoni, nagundua ya kwamba, matatizo yao yanahusiana moja kwa moja na kutofuata ama kutozingatia miiko ya jinsi ya kushughulika na habari za wafu.
Ninapo zungumzia habari za wafu, namaanisha masuala yoote yanayo husiana na wafu, kuanzia makaburi, maiti, vyumba vya kuhifadhia maiti, taratibu za kumuandaa na kumuosha marehemu, taratibu za maziko na mazishi, taratibu za matanga & maombolezo, nguo za marehemu, masuala ya mirathi ya marehemu, jinsi ya kuishi na yatima walio achwa na marehemu, mke au wake za marehemu , mali za marehemu nakadhalika.
Watu wengi wana pata nuksi, mikosi au hata vifo visivyo vyao, kwa sababu ya kutozingatia taratibu za namna ya kushughulika na wafu.
Somo hili lina muhusu kila mmoja wetu, kwa sababu kila mtu anaweza kupata msiba wa ndugu, jamaa au rafiki wakati wowote ule.
Pamoja na kwamba, hakunaga mtu mwenye uzoefu wa kufiwa. ( Yaani kuzoefu uchungu wa kufiwa kwa sababu umeshapata misiba mizito mingi ), lakini linapokuja suala la kufahamu kuhusu miiko na taratibu za namna ya kushughulika na habari za wafu, kila mtu anapaswa kuwa na uzoefu wa kutosha, kwa sababu msiba unaweza kuja wakati wowote.
Ni muhimu sana kujua taratibu na miiko ya namna ya kushughulika na habari za wafu ili usije kupata madhara yasiyo ya lazima, kwa sababu ya kutokujua nini cha kufanya pale unapokuwa una shughulika na habari za wafu.
Kwa bahati mbaya sana, nyakati za siku hizi hata watu wazima nao hawajui namna ya kushughulika na habari za wafu. Kupitia mfululizo wa makala haya, nitakuwa nikielezea kuhusu miiko mbalimbali ya namna ya kushughulika na habari za wafu.
Fuatilia makala haya mwanzo hadi mwisho, ili upate kuzijua taratibu hizo na hivyo kujiepusha na madhara mbalimbali yanayo weza kukupata kutokana na kutokujua kwako.
1. KAMA UMEJIFUNGUA MTOTO AMBAE AMEZALIWA AKIWA AMESHA KUFA TAYARI
Moja kati ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo makini sana, ni pale unapokuwa una shughulika na mazishi ya kichanga, hususani kile kilicho zaliwa kikiwa kimekufa tayari.
Hii ni kwa sababu, maiti ya vichanga, pamoja na eneo vinapozikwa vitoto vichanga ni hazina kubwa sana katika ulimwengu wa wachawi na walozi.
Katika ulimwengu wa wachawi na walozi, watoto wachanga walio zaliwa wakiwa wamekufa tayari, hujulikana kama “ WATU WALIO PITA DUNIANI BILA KUONEKANA” .
Wachawi wanapo sikia mwanamke amejifungua kitoto kichanga kikiwa kimefariki dunia, hukusanyika na kufanya karamu kubwa ya kichawi, kwa sababu , maiti ya kitoto kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimefariki dunia, ina maana kubwa sana katika shughuli zao.
Wachawi hutumia vitovu vya watoto wachanga walio zaliwa wakiwa wamekufa, kama malighafi ya kutengeneza aina mbalimbali za ndumba za kichawi, mfano; kutengeneza ndumba ya kuwafanya wasionekane na maadui zao, kutengeneza uchawi wa kuiba na kufunika nyota ya mtu au biashara ya mtu na kumfanya mtu huyo pamoja na biashara yake visonekane hadi anaingia kaburini, kutengeneza mafuta yajulikanayo kama mafuta ya usiku, ambayo hutumiwa na wafanyabiashara hasa wafanya biashara ndogo ndogo katika kuvuta wateja kwenye biashara, kutengeneza filimbi ya kichawi ambayo hutumika kuwaita wachawi kwenye mikutano yao ya kichawi.
Wachawi hutumia kufanya matambiko mazito kwenye makaburi yaliyo tumika kuzika vitoto vichanga ambayo mara nyingi huwa yanakuwa majumbani.
Matambiko hayo ya kichawi, huwa na madhara makubwa sana kwa watu wanaoishi katika nyumba hiyo, hususani wazazi pamoja na ndugu wa hicho kichanga.
Endapo wachawi watafanikiwa kutumia katika shughuli zao za kichawi, maiti ya kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, mabalaa, nuksi na mikosi mbalimbali itaiandama familia ya kichanga hicho, kwa sababu moja kati ya maunizi yanayo fanywa na wachawi, huwa ni pamoja na kuwatupia mikosi wazazi wa kichanga hicho, hususani mama wa kichanga hicho.
Wachawi watatumia tambiko la kitoto hicho kichanga kama lango la kichawi la kuingia katika familia ya wazazi wa kitoto hicho na kuifanya kama watakavyo.
Moja kati ya dalili kwamba, wachawi wametumia katika shughuli zao za kichawi, kitoto chako kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, ni pamoja na kutopata ujauzito , kubeba mimba zinazochoropoka, au kuendelea kuzaa vitoto vilivyo kufa, katika kila ujauzito unao upata.
NINI CHA KUFANYA : 1. Kwanza unapokuwa mjamzito unatakiwa kuchukua tahadhari ya hali ya juu sana ili kuepuka kuzaa kitoto ambacho kimekufa, kwa sababu wachawi huwa wanawafunga wanawake wajawazito wajifungue vitoto vilivyo kufa ili waweze kuvitumia katika mambo yao ya kichawi.
Hivyo unapokuwa na mke mjamzito, hakikisha unampa kinga madhubuti ambayo itawazuia wachawi kumfunga na kusababisha kichanga hicho kisicho na hatia, kuzaliwa kikiwa kimepoteza maisha. 2. Kama tayari umejifungua kitoto ambacho kimezaliwa kikiwa kimeshakufa, unatakiwa ufuate taratibu maalumu za kukifanyia maziko maalumu, pamoja na wewe mwenyewe kufanyiwa tambiko maalumu la kukusafisha na kukukinga dhidi ya jambo kama hilo, katika siku zako zijazo.
Taratibu za maziko ya vitoto vichanga vilivyo zaliwa vikiwa vimekufa, zinategemea na mambo makuu yafuatayo : jinsia ya mtoto, siku aliyo zaliwa mtoto, mtoto amezaliwa peke ake au wamezaliwa mapacha, kama ni mapacha wamekufa wote au mmoja amepona, na kama mmoja amepona, zipo pia taratibu za namna ya kumfanyia tambiko na ibada maalumu ili kumuepusha na jicho la maadui wa kichawi.
Kitu kingine, inategemea na mtoto aliyezaliwa ni NZAO ama UZAO wa ngapi wa mwanamke aliye jifungua. Kama ni uzao wa kwanza, kuna taratibu zake, na kama ni uzao wa mwisho kuna taratibu zake pia.
Taratibu hizi zisipo fuatwa, basi madhara makubwa sana yatatokea kwa familia husika.
2. KAMA MAMA AMEFARIKI NA MTOTO AMEBAKI HAI
Kama utapatwa na mtihani huu, unapaswa kuwa makini sana na kuzingatia taratibu na kanuni za kufuata.
Ninaposema kuwa makini namaanisha uwe makini kwelikweli, kwa sababu wachawi wana siri kubwa sana na mwanamke aliye jifungua na kufariki dunia.
Kuwa makini sana na watu watakao enda kuuosha mwili wa mke wako ,au dada yako n.k ambae amefariki wakati anajifungua, kwani baadhi yao watakuwemo wachawi ama mawakala wa wachawi ambao watachukua baadhi ya vitu vya mke wako na kwenda kuviuza kwa wachawi.
Vitu hivyo ni pamoja na nywele, nywele za sehemu za siri, kucha, na maji yaliyo tumika kumuoshea.
Vitu hivyo hutumiwa na wachawi kutengeneza ndumba za aina mbalimbali, kama vile kuwafunga wanafunzi wanao soma, wafanyakazi, wafanya biashara nakadhalika.
3. KAMA MAMA NA MTOTO WOTE WAMEFARIKI:
Kama kwa bakti mbaya umepatwa na mtihani mzito kama huu, unapaswa kuwa makini na kuchukua tahadhari kama ilivyo elezwa hapo juu.
4. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KICHAA AU MWENDAWAZIMU
Kama ndugu yako aliyefariki alikuwa kichaa au mwendawazimu wakati wa uhai wake na alifariki dunia akiwa katika hali hiyo unapaswa kuzingatia yafatayo :
Kwanza maiti yake isilale ndani. Itoke moja kwa moja mochwari hadi makaburini. Nguo zake zote zichomwe moto siku ya saba baada ya maziko.
Kuweni makini sana na watu watakao enda kuosha mwili wake.
Ikiwezekana awepo mwanafamilia anae aminika, wakati wa zoezi la kuuosha mwili wa ndugu yenu, kwa sababu watu walio kufa wakiwa wendawazimu ni hazina kubwa sana kwa wachawi, kuanzia sehemu za miili yao, hususani nywele na kucha, nywele za siri , sanda iliyo tumika kuwavisha, nguo walizokuwa wamevaa wakati wa kupatwa na umauti pamoja na kaburi lililo tumika kuwazika.
Wachawi hutumia vitu hivyo katika kutengeneza uchawi na ulozi wa aina mbalimbali.
Kwa mfano, nywele za marehemu ambae alikuwa mwendawazimu wa jinsia ya kiume, hutumika kutengeneza ndumba ya kichawi ya kumtuliza kimapenzi mwanaume na kumfanya awe kama mwendawazimu kwa mwanamke aliye mfanyia uchawi huo.
Vivyo hivyo, nywele za mwanamke aliyefariki akiwa mwendawazimu hutumika kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza wanawake kimapenzi na kuwafanya kuwa kama wendawazimu kwa waume zao.
Kama hiyo haitoshi, wachawi huchukua nywele za marehemu mwendawazimu wa kiume, huchanganya na nywele za mwendawazimu mwanamke, nywele za mtu aliyekufa akiwa msukule, mafuta ya msukule pamoja na ndumba nzingine, ili kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza na kuwafunga wafanyakazi hususani wale wanao fanya kazi kwenye kampuni za watu binafsi.
Uchawi huu hutumiwa sana na matajiri wanao miliki maduka, hoteli, migahawa au kampuni zao binafsi.
Mtu aliye fanyiwa uchawi huu mara nyingi huwa na uwezo mkubwa na wa kipekee katika kazi yake, na bosi wake anakuwa hayupo tayari kupoteza huduma yake, basi anacho kifanya ni kumlisha uchawi huu na kumpumbaza katika maisha yake yote.
Vilevile, wachawi hutumia vitu vya mwendawazimu kutengeneza uchawi wa biashara hususani biashara ya chakula .
Mtu ukishakula tu chakula kilicho wekwa uchawi huu basi utakuwa kama mwendawazimu kwenye chakula cha kwenye mgahawa au hoteli hiyo.
Huwezi kula chakula sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa kwenye mgahawa huo tu, hata yatokee mabadiliko gani.
Uchawi huu pia hutumiwa na wafanyabishara wa biashara nyinginezo kama vile nguo nakadhalika. Kumpumbaza mteja. Mteja huweza kununua nguo ambayo thamani yake ni sh elfu kumi, kwa shilingi laki moja.
Uchawi huo ndio unao tumiwa sana na akina dada katika kuwapumbaza wanaume na kuwafanya wawape kila kitu wanacho kitaka. Endapo utaruhusu wachawi watumie vitu vya marehemu ndugu yenu ambae amefariki akiwa mwendawazimu, basi mikosi na mabalaa makubwa yataiandama familia yenu.
5. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KIPOFU !
Unapaswa kuwa makini sana, pale unapopatwa na msiba wa ndugu yako wa damu ambae alikuwa na ulemavu wa kutokuona yaani kipofu.
Hii ni kwa sababu wachawi wanaweza kutumia katika shughuli zao za kichawi baadhi ya vitu vya ndugu yenu na matokeo yake kuiacha familia yenu ikiwa kwenye mabalaa na mikosi isiyo elezeka.
Kuweni makini sana na aina ya watu watakao pewa jukumu la kuosha mwili wa ndugu yenu.
Nawashauri badala ya kuwapa kazi hiyo watu wa mochwari, ifanye ninyi wenyewe ili kuhakikisha kuwa hakuna ufisadi wowote unao fanyika hapo.
Kwani endapo hamtafanya hivyo, basi mtatoa nafasi kwa wachawi pamoja na wakala wao kuchukua baadhi ya vitu vya ndugu yenu huyo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kichawi.
Vitu hivyo ni pamoja na nywele, nyusi,nywele za siri,kucha, nguo alizokuwa amezivaa marehemu wakati anaaga dunia, kama alikuwa anatumia gongo la mti, nalo ni dili kubwa sana kwa wachawi, maji yaliyo tumika kumuosha nakadhalika.
Pamoja na mambo mengine, vitu vya marehemu ambae wakati wa uhai wake alikuwa na ulemavu wa kuona yaani upofu ( Hasa Yule aliye zaliwa na upofu ), hutumiwa na wachawi kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile uchawi wa kuwafunga maadui zako wasi kuone, uchawi wa mapenzi kumfanya mpenzi wako asimuone mtu mwingine yoyote Yule isipokuwa wewe tu, kufunga nyota ya mtu isionekane na yoyote Yule. Kwenye kaburi la marehemu aliyekuwa na ulemavu wa kuona, hufanyika tambiko la kuzika na kufunga kesi, kuifanya isionekane.
Pia vitu hivyo hutumika kuwaloga wanawake wajawazito kuzaa watoto wenye ulemavu wa macho
6. KAMA NDUGU ALIYE KUFA ALIKUWA NA ULEMAVU WA KUTOSIKIA :
Wachawi hutumia vitu vya mtu aliye fariki ambae wakati wa uhai wake alikuwa na ulemavu wa kusikia, kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile; Mapenzi; kumfanya mpenzi asisikie jambo la mtu yoyote Yule, isipokuwa wewe tu, kumroga mtoto wa mtu kumfanya asiwasikie wazazi wake, kumroga mke au mume wa mtu kufanya asiwe na masikizano na mwenzi wake nakadhalika.
Vitu vinavyo tumika hapo ni pamoja na nywele, nyusi, kucha, nywele za siri, nguo zake, maji yalotumika kumwosha pamoja na kaburi lake.
Unapopatwa na msiba wa ndugu ambae wakati wa uhai wake alikuwa na tatizo la ulemavu wa kusikia, basi unapaswa kuwa makini sana.
7. KAMA NDUGU YENU AMEKUFA MAJI : Kama mmepata taarifa kuhusu msiba wa ndugu yenu ambae amekufa maji, eidha alikuwa anaogelea, au amepata ajali kwenye mashua au jahazi au meli, zipo taratibu na miiko ya kufuata wakati wa maziko yake.
Moja ya miiko hiyo ni pamoja na “ msichimbe kaburi kabla hamjaupata mwili wa marehemu”.
Hakikisheni kwanza mmeupata mwili wake ndio mchimbe kaburi na kumzika kwa kufuata taratibu zote za kumzika mtu aliye fariki kwenye ajali ya maji.
Msichimbe kaburi kabla hamjauona mwili wa marehemu. Endapo mtachimba kaburi kabla ya kuuona mwili wa marehemu halafu ikatokea bahati mbaya msiupate mwili wa marehemu, basi kwanza, mmoja kati ya ndugu wa karibu katika familia ya marehemu, atafariki dunia ndani ya mwaka huo huo. Idadi ya ndugu watakao fariki ndani ya mwaka mmoja, itategemeana na idadi ya siku ambazo hilo kaburi limekaa wazi.
Kama hiyo haitoshi, pili , mtakuwa mmewapa faida kubwa sana wachawi.
Wachawi wataenda kulitumia kaburi hilo kutengeneza uchawi mkubwa na wenye nguvu sana.
Makaburi ya namna hiyo hapa Afrika mashariki yapo machache sana, na yanapatikana zaidi nchini Congo DRC na Tanzania hususani kanda ya ziwa na kanda ya kusini katika mkoa wa Lindi.
Kanda ya ziwa makaburi hayo yapo katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu, na mengi kati yao ni yale ya wahanga wa ajali ya meli ya MV Bukoba ya mwaka 1996, ambapo mamia ya miili ya abiria waliokuwa kwenye meli hiyo haikuweza kupatikana, ilihali ndugu, jamaa na marafiki walisha chimba makaburi.
Huko nchini Kongo, idadi kubwa ya makaburi hayo ni yale ya wale mabinti bikira, walio kufa kwenye ajali ya meli iliyotokea mto Kongo miaka ya 70.
Katika ajali hiyo hakuna, mwili uliopatikana hata mmoja na idadi kubwa ya ndugu, jamaa na marafiki wa mabinti hao ilikuwa tayari imeshachimba makaburi kwa ajili ya kuwahifadhi wapendwa wao hao. LAWAMA NYINGI KUHUSU AJALI HIYO ZILIELEKEZWA KWA ALIYE KUWA RAIS WA KONGO KIPINDI HICHO, MOBUTU SSESESEKO AKIDAIWA KUWATOA KAFARA MABINTI HAO KWA MAELEKEZO YA KAMATI YAKE YA UFUNDI ( Miiko yangu ya kazi, hainiruhusu kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili )
8. MSICHIMBE KABURI HALAFU LIKALALA BILA KUZIKWA : Kaburi huwa halilali njaa, hakikisheni siku mtakayo chimba kaburi hilo, iwe ndio siku mtakayo mzika marehemu wenu.
Kamwe msichimbe kaburi kabla mwili haujafika nyumbani.
Endapo mtakiuka jambo hilo, basi misiba itaiandama familia yenu kwa mwaka mzima.
Mtakuwa mmeiunganisha familia yenu na kaburi lililo lala wazi kwa hiyo siku moja. Tumbo la kaburi hilo litadai malipo yake ya kulala bila chakula chake kwa siku nzima.
9. MSIACHE KABURI WAZI WAKATI MNAENDA KUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU
Mkishamaliza kuchimba kaburi, msilitelekeze peke yake. Wekeni watu kadhaa wa kulinda kaburi ambao watakaa huko kaburini hadi pale mwili wa marehemu utakapo letwa kuzikwa.
10. MWANAMKE MJAMZITO ASIHUDHURIE MAZISHI Mwanamke mjamzito hatakiwi kuhudhuria kwenye maziko ( makaburini ).
Endapo atafanya hivyo basi, roho ya marehemu itamuingia mtoto aliyeko tumboni, na hivyo kusababisha bahati mbaya na mikosi kwa mwanamke huyo wakati wa kujifungua na endapo atajifungua salama, basi mtoto atakae zaliwa anaweza kupoteza uhai, au endapo ataishi basi, mama huyo atafariki na kumuacha motto na motto atakuwa kwa taabu sana na ataandamwa na mikosi.
Kama itatokea mwanamke huyo akalazimika kuhudhuria kwenye mazishi ( Mfano labda aliyefariki ni mtu wake wa karibu sana kama vile mama yake,baba yake, mume wake, kaka yake, dada yake au mtoto wake ), basi anatakiwa ASITAZAME MWILI WA MAREHEMU wakati wa kuaga.
Endapo atafanya hivyo, basi ile roho ya marehemu itaishaishawishi roho ya mtoto aliyepo tumboni, kwenda kwenye nchi ya wafu, jambo ambalo litasababisha matatizo makubwa sana kwa mama wa mtoto wakati wa kujifungua.
Uwezekano wa kujifungua mtoto aliyefariki, utakuwa kwa asilimia mia.
11. Unapopita kwenye eneo la makaburi mida ya saa saba mchana au saa moja usiku, usiache mdomo wako wazi wala kupiga miayo. Endapo utafanya hivyo, roho za wafu zitakuingia na kusababishia matatizo makubwa.
12. Mnapomzika marehemu, kichwa kiangalie upande wa magharibi na miguu iwe upande wa mashariki.
14. Mara tu kifo kinapotokea, kitu cha kwanza, unacho takiwa ni kuondoa ama kufunika picha na vioo vyote vilivyomo kwenye chumba alichopo marehemu. Ni nuksi kubwa sana kuacha taswira ya mwili wa marehemu ionekane kwenye kioo. Kama hiyo haitoshi, ni nuksi kubwa sana kutazama taswira yako kwenye kioo hicho, mpaka mwili wa marehemu uatakapo kuwa umeondolewa. Ukitaka kuamini ninacho kisema, jaribu kuingia na kioo kwenye chumba alimo lala marehemu halafu jitazame kwenye hicho kioo. Utakacho kiona, uje ukisimulie hapa.
15. Naweni mikono kwa dawa maalumu baada ya kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu.
16. Oga dawa mara baada ya kutoka kaburini.
17. Kama marehemu amefariki akiwa nyumbani, mnapoenda kuutoa mwili wake, miguu itangulie kutoka, kamwe msifanye kosa mkatanguliza kichwa.
18. Kama watu wawili katika nyumba moja, wanaumwa sana, halafu ikatokea mmoja wao akafariki dunia, basi hiyo ni ishara kwamba huyo mwingine atapata nafuu kubwa.
19. Kuna ndege mmoja anapatikana porini ( SIMTAJI KWA SABABU ZA KIMIIKO), ukichukua nyoya la huyo ndege halafu ukaliweka kwenye mto wa kitanda anacho lalia mgonjwa, basi mgonjwa huyo atakufa wala hatopona. Nyoya hilo hilo likiwekwa kwenye kitanda anacholalia mtoto mdogo, litamzuia mtoto huyo kukua.
20. Kitanda anacho lalia mgonjwa mahututi, kitazame mashariki na magharibi, na kamwe sio kaskazini na kusini. Kichwa kiangalie magharibi na miguu itazame mashariki.
21. Jina la mwisho kutajwa na marehemu wakati anakaribia kukata roho, litakuwa jina la mtu atakae fuatia kufa baada ya marehemu.
22. Endapo mtu anae karibia kukata roho, atakun’gata, basi na wewe utamfuata baada ya muda mfupi. Ili kujiepusha na kifo cha namna hiyo, basi unatakiwa na wewe umng’ate katika sehemu ile ile aliyo kun’gata.
23. Kama kiongozi wa familia atafariki dunia, basi mnatakiwa kusimamisha saa kubwa ya ukutani inayo kaa sebuleni, vinginevyo wanafamilia walio baki nao watamfuata ndani ya kipindi kichache, vitatokea vifo mfululizo vya wanafamilia.
24. Baada ya kuuosha mwili wa marehemu, na kuuvisha nguo zake, unatakiwa kuweka punje moja ya chumvi kwenye kifua cha marehemu ili kuwafukuza roho na majini wabaya.
25. Kama marehemu atakuwa akiwa ameacha macho wazi , hiyo ni ishara mbaya sana. Maana yake ni kwamba,anatafuta watu ( ndugu zake ) wa kwenda nae kaburini. Kujiepusha na hilo, funikeni macho yake kwa kutumia sarafu .
26. Usifagie chumba cha marehemu kabla marehemu hajatolewa. Endapo utafanya hivyo, basi amini nakwambia wewe ndie utakae mfuata marehemu.
27. Msitoe shuka wala nguo yoyote iliyopo kwenye kitanda alicho kilalia marehemu, na ambacho umauti ulimkuta. Endapo mtakiuka hilo, basi mwanafamilia mwingine atafariki ndani ya mwaka huo huo.
28. Endapo Kundi la wanandugu, jamaa na marafiki, mtaenda kuuchukua mwili wa marehemu halafu ghafla mkaona anatoa damu kwenye tundu za pua, basi mjue kuwa marehemu amekufa kwa mkono wa mtu, na aliye husika na kumuua, yu miongoni mwenu,ndani ya chumba hicho hicho.
29. Kwa mara nyingine tena narudia, mwili wa marehemu unapotolewa kwenye jengo lolote lile, iwe nyumbani, kanisani, au msikitini ni lazima miguu ndio itangulie kutoka na sio kichwa, vinginevyo roho au mzimu wa marehemu huyo, utatazama katika jengo hilo na kumuita mtu mwingine wa kufuatana nae.
30. Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.
31. Ukiugusa mwili wa marehemu, utakuwa na uhakika kwamba, roho ya marehemu haitakusumbua. Na endapo utaugusa mwili wa marehemu usoni, hutoota ndoto mbaya kuhusu marehemu huyo.
32. Usipeleke mwili malaloni kwa kutumia gari lako binafsi. Ni nuksi kubwa sana kufanya hivyo. Mwili wa marehemu unapelekwa malaloni kwa kutumia gari maalumu.
33. Endapo mtasafirisha mwili wa marehemu kwa basi, kichwa kitazame anapotoka na miguu itazame anapoelekea.
34. Usi hesabu magari kwenye maziko (makaburini), ukifanya hivyo unakuwa unahesabu siku zako mwenyewe za kuishi.
35. Kuwa muangalifu usione taswira yako kwenye gari lililo beba mwili wa marehemu, vinginevyo wewe ndio utakae fuatia kubebwa kwenye gari hilo.
36. Usiende na mtoto mchanga kwenye msiba, vinginevyo atakufa kabla hajatimiza mwaka mmoja.
37. Ni nuksi kubwa sana kutangulia makaburini ( kwenye maziko) au kupita bila kushiriki kwenye maziko . Kama utafanya hivyo, utakufa ndani ya muda si mrefu.
38. Kama paka mweusi atakatisha mbele wakati wa maziko (makaburini ) mwanafamilia mmoja katika familia ya marehemu atakufa ndani ya siku tatu.
39. Kama ndugu yenu amekufa, kwa kuuwawa au mna wasiwasi kwamba ndugu yenu ameuwawa, basi mzikeni huku kichwa kikiwa kinatazama chini. Mtu aliye muua ndugu yenu, kama atakuwa kwenye eneo la maziko, basi hatoondoka eneo hilo hadi atakapo kamatwa. Watu wote wataondoka, lakini yeye atabaki, hapo hapo, atakuwa kama amepagawa na kupigwa na bumbuwazi. Kama msiporudi kutazama hapo kaburini, basi hata siku tatu mtamkuta, na atakapo waona, basi ata tubu na mtafikisha kwenye vyombo vya dola.
Miaka ya sabini kushuka chini, babu zetu ilikuwa kama ndugu yao amekufa kwa kuuwawa ama kama wanahisi ndugu yao amekufa kwa kuuwawa, mfano amewekewa sumu, amenyongwa n.k,. basi walikuwa wanafanya hivi, wanatoa ini la marehemu, halafu wanazika ini sehemu tofauti na mwili wa marehemu, kwa kufanya tambiko maalumu. Ndani ya siku saba, mtu aliye muua marehemu, atapatikana katika eneo lililozikwa ini.
40. Kaburi lilisale wazi, likilala wazi, basi mwanafamilia mwingine katika familia ya marehemu atafariki ndani ya mwaka huo huo. Kaburi lizikwe siku liliyo chimbwa.
41. Kaburi likilala wazi siku ya Jumapili, basi jumapili itakayo fuata, mwanafamilia mwingine kutoka kwenye familia ya marehemu na yeye atamfuata marehemu.
42. Vifaa vilivyo tumika kuchimba kaburi, vinatakiwa vibakie kaburini kwa siku nyingine saba. Kuvipeleka nyumbani vifaa hivyo siku hiyo hiyo aun kabla ya siku saba, ni nuksi kubwa sana.
43. Kuondoka makaburini kabla kaburi lote halijafukiwa, kutasababisha msiba kwenye familia yako wewe uliye ondoka kabla watu hawajamaliza kuzika. Mvua ikinyesha kwenye kaburi ambalo bado halijafukiwa, ni ishara mbaya sana kwa familia ya wafiwa. Ili kuepukana na nuksi hiyo, inabidi kuwe na mtaalamu wa kuzuia mvua.
44. Ni nuksi kubwa sana kusonta kaburi
45. Ni nuksi kubwa sana kurukia kwenye kaburi
46. Ni nuksi kutembelea makaburini baada ya jua kuzama
47. Wafiwa wasiondoke nyumbani wala kujichanganya mtaani na watu wengine, hadi matanga yatakapo inuliwa. Kwa mfano watu wengine, unakuta mtu amefiwa, lakini kabla hata matanga hayajainuliwa, anakwenda bar kunywa na kurudi msibani. Hayo ni makosa makubwa sana.
48. Wafiwa wote wakuu, yaani ndugu wa karibu wa marehemu, wasioge hadi baada ya siku tatu, ambayo ndio siku ya kuanua matanga, na maji watakayo oga yawe maji ya moto.
49. Wafiwa wasishiriki ngono hadi matanga yatakapo inuliwa.
50. Waombolezaji msibani, wasiongee kwa nguvu wala kucheka kwa nguvu. Ni makosa makubwa sana kufanya hivyo.
Leo tumekomea miiko 50. Kama kichwa cha maya kinavyo jieleza, MIIKO ELFU MOJA NA MOJA YA WAFU. Hivyo basi, ili kufahamu kuhusu miiko mingine iliyo baki, tembelea kila siku: www.mungwakabili.blogspot.com
Imesimuliwa na Dokta. mungu wa kabili. Anapatikana kwa simu namba 0744 000 473
Post a Comment