Mwanamke Afukua kaburi la mtoto wake na kuchukua maiti

MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Luth Sekeleketi  mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi  kwa  tuhuma za kufukua  kaburi  alilozikwa mwanae baada ya kufariki, na kuchukua mwili  akiamini ataombewa na wachungaji  na kufufuka.

Tukio hili la kusikitisha na kustaajabisha limetokea katika kijiji cha Shigamba Mbalizi  Mkoani Mbeya ,ambapo inadaiwa kuwa marehemu huyo aliyefahamika kwa jina la Baraka Mwafwongo amefariki dunia februali 16, na baada ya siku moja tangu azikwe mwanamke huyo ambaye ni mama mzazi wa marehemu , amefukua kaburi na kuuchukua  mwili wa marehemu, kisha kuuhifadhi kwenye pagala la nyumbani kwake, kwa madai kuwa atafufuka ,jeshi la polisi limelazimika kufukua kaburi ili kujiridhisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya , Naibu Kamishna wa Polisi Dhahiri Athuman Kidavashari anasema, mwili huo umepelekwa katika hospital teule ya Ifisi na taratibu nyingine za kisheria zitafuatwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hili wanasema mwanamke huyo aliufukua mwili huo akishirikiana na vijana wawili na kuuhifadhi nyumbani kwake , kwa imani kwamba mtoto wake atafufuka.

Channel Ten ikazungumza na mwanamke huyu ambaye amefukua kaburi na ku chukua mwili wa mtoto wake  na haya ni baadhi tu ya maelezo yake.

Mkuu wa Wilaya ya  Mbeya Willium  Paul Ntinika akawataka wachungaji kuacha tabia ya kuwadanganya waumini wao.

Post a Comment

[blogger]

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.