Mapema Jioni ya Jumamosi ya Tarehe 4, 2017. Ilisambaa taarifa inayoanisha Majina Kadhaa ya watu maarufu hapa Bongo ikisema kuwa ni miongoni mwa watu waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi jijini dar siku ya Jumatatu kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda na Jeshi la Polisi kuhusiana na Sakata la uuzaji na Utumiaji wa Madawa ya Kulevya nchini.
Katika majina hayo yaliyotolewa na Taarifa hiyo ambayo haikuonesha nani mtoaji wa taarifa hiyo bali ikionyesha Anuani tu ya Jeshi la Polisi nakuleta walakini wa taarifa hiyo ni Jina la Msanii Maarufu na Mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa nchini Tanzania Diamond Platnumz ambapo kwenye taarifa hiyo ameandikwa kwa jina la Nasibu Abdul.
Taarifa iliyo Sambaa Mtandaoni
Meneja wa Msanii huyo Babu Tale ameona sio sawa kukaa kimya na ameweza kujibu kwa ufipi sana na kusema kuwa "No Information, No right to speak!!! Marry you - link on my bio". Amepost kupitia mtandao wa Picha wa Instagram.
Post a Comment