Yapo Mengi Lakini Haya ni Matukio Matano Yaliyoishangaza Dunia

 Kulipuliwa kwa Majengo ya Biashara (WTC) jijini New York

KUNA mambo mengi yamekuwa yakitokea duniani, yanashangaza na wakati mwingine mtu kujiuliza kwamba inawezekanaje jambo hilo kutokea? Tangu dunia ilipoumbwa, kuna mambo mengi yalitokea kuanzia karne ya 18 mpaka karne hii ya 21.

Yapo yaliyotokea kwa makusudi lakini pia yapo yaliyotokea kwa bahati mbaya kabisa ambayo kwa kifupi tungesema Mungu alitaka hayo yatokee ili iwe fundisho kwa watu wanaoshuhudia au akusikia. Haya hapa ni baadhi ya mambo matukio matano ambayo yaliishangaza dunia.
Ilikuwa asubuhi ya tarehe 11/09/2001. Wafanyakazi walikuwa ndani ya majengo mawili ya biashara (WTC) wakiendelea na kazi zao kama kawaida. Ghafla waliiona ndege ya kwanza ikienda kwa kasi katika jengo leo.

Walipiga kelele, walishangaa kwani haikuwa kawaida kwa ndege kutoka uwanja wa ndege na kulifuata jengo moja na kuligonga. Walikufa watu wengi na wengine kuachwa majeruhi. Wakati watu wakijiuliza ni kitu gani kilitokea, ghafla ndege ya pili ilionekana ikilifuata jengo jingine ambalo ni pacha ya lile la kwanza na kuligonga.

Kwa taarifa za CIA, hii haikuwa bahati mbaya, lilikuwa ni tukio lililopangwa, la kigaidi ambalo lilifanywa na Kundi la Kigaidi la Al Qaeda lililokuwa chini ya Osama Bin Laden. Katika tukio hilo kubwa, liliua watu 2996 na kujeruhi watu 6000 na kuleta hasara ya dola trilioni 3.

 Kulipuliwa kwa Miji ya Nagasaki na Hiroshima.

Ni mwaka 1945 ambapo Vita vya Pili vya Dunia (WWII) vilikuwa vimepamba moto. Mataifa mengi yakaungana kwa ajili ya kushambuliana huku Ujerumani iliyokuwa chini ya Adolf Hitler ikiwa imeungana na Italia, Japan na nchi nyingine.

Zilikuwa zikipambana na kundi jingine lililokuwa na nchi kama Uingereza, Ufaransa na nchi nyinginezo. Vilikuwa vi vita vikali, walipambana kwa nguvu kubwa na ndiyo ilikuwa vita pekee ambayo Marekani aliitumia kutengeneza nchi yake.
Wakati wenzake wakiwa kwenye vita, kazi yake ilikuwa ni kuitengeneza nchi, alikuwa akiwauzia Waingereza na wenzao nguo, chakula na silaha. Vita viliendelea mpaka pale ndege ya Marekani ilipolipuliwa na Japan kitu kilicholeta mtafaruku mkubwa kwamba kwa nini Japan ailipue ndege hiyo, huku japan akiinuka na kusema kwamba kwa nini Marekani awauzie Waingereza silaha na chakula na wakati yeye hakuhusika kwenye vita hivyo?

Japan hakubaki kimya, alidhamiria kumuingiza Marekani katika ugomvi huu kwa kushambulia miji kadhaa nchini Marekani. Hapo ndipo rais wa Marekani Harry S. Truman alipouliza kuhusu silaha walizokuwanazo na kuambiwa kwamba walikuwa na mabomu mawili ya nyuklia na yalikuwa hatari sana. Akaagiza hayohayo yaende kushambulia Miji ya Nagasaki na Hiroshima nchini Japan. Kilichotokea huko, hakika Wajapan hawatokisahau na kuanzia siku hiyo, hawakutaka tena vita.

Kifo cha John F Kennedy

Ni mwaka 1963 ambapo Rais wa 35 wa Marekani, John F Kennedy alikuwa kwenye msafara wake uliokwenda kutembelea Jiji la Dallas, Texas. Wakati akiwa na mkewe kwenye gari lililokuwa wazi kwa juu, jamaa mmoja aliyeitwa Lee Harvey Oswald (Mdunguaji) alikaa kwenye ghorofa akiwa na bunduki yake kisha kumpiga risasi Kennedy kwenye kichogo na kufariki hapohapo.

Huyo alikuwa rais wa mwisho wa Marekani kuuawa na tangu siku hiyo wakatangaza kwamba hakutokuwa na rais wao yeyote atakayeuawa, hivyo wakaongeza ulinzi maradufu. Kwa muuaji Oswald, alikamatwa ila kabla ya kupewa hukumu yake, akauawa gerezani kwa kitu kilichohusishwa kwa kupoteza ushahidi.

 Mwanadamu wa kwanza kufika mwezini

Hebu usiku toka ndani na kwenda nje, kisha angalia angani, bila shaka utauona mwezi, si upo mbali, basi nataka nikwambie kwamba katika matukio yaliyowahi kuishangaza dunia ni kitendo cha binadamu wa kwanza kufika huko.

Ilikuwa mwaka 1968, Mmarekani, Neil Armstrong alipoamua kufika mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Ilionekana kama kushindikana lakini mwisho wa siku mtu huyo alifika huko na kukaa kwa saa 21. Alipofika, kwanza hakutoka nje ya chombo hicho kwa muda wa saa sita, alibaki ndani huku akijiuliza kama alitakiwa kutoka au la, ila mwisho wa siku akatoka.

Dunia iliweka historia, kila mtu akamuona Armstrong kuwa shujaa mkubwa ambaye alifanya kile ambacho binadamu wengine waliona kwamba isingewezekana hata kidogo. Baada yake, kulikuwa na watu wengine waliokwenda. Kwa sasa, watu wanafikiria kwenye sayari ya Mars.

Kuzama kwa meli ya Titanic

Ilikuwa mwaka 1912 siku ambayo meli ya Titanic ilitakiwa kuanza safari yake kutoka Southampton nchini Uingereza na kwenda New York nchini MArekani.

Ilikuwa meli kubwa na watu walioitengeneza walijivunia kwa kusema kwamba isingeweza kuzama kwani ilikuwa imara sana, tena sana.

Meli hii ilibeba abiria 2224 na ilipozama siku nne baadaye iliua abiria 1635. Mara baada ya taarifa kutangazwa, watu wengi walishtuka kwani waliamini kwamba kwa ukubwa wa meli hiyo, uimara wake usingeweza kuzama hata mara moja na waliamini kwamba ingefanya safari ndefu kuliko meli zote.

Meli hiyo ilizama baada ya kugonga mwamba wa barafu katika Bahari ya Atlantiki inayotenganisha Marekani na Bara la Ulaya.








Visit website

Post a Comment

[blogger]

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.