PSG VS BARCELONA.. UCHAMBUZI


Usiku mzuri unarejea, usiku wa kipekee, usiku unaowaweka watu wote wapenda soka sehemu moja. Hakuna asiyetaka kuona PSG ya Unai Emery dhidi ya akili za Luis Enrique. Bahati nzuri kubwa kwenye mchezo huu ni kuwa timu hizi zimekutana mara 9 tayari, hivyo ni kama wamezoeana.

PARIS ST GERMAIN

Ni timu mpya tofauti na ile iliyokutana na Barcelona kipindi cha nyuma. Ni wepesi zaidi kutokana na kutumia mshambuliaji mmoja zaidi kwa wakati huu (Cavani) ambaye ni mwepesi kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine huku kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic kukiwa kumempa uhuru zaidi. Huyu amefunga mabao 33 tayari kwenye mashindano yote msimu, amekuwa hatari kwelikweli. Walau ameonyesha thamani aliyonunuliwa nayo kule Napoli.

BARCELONA

Kuna nyakati wameonekana kama wanakosa ukali waliokuwepo nao takribani misimu mwili iliyopita. Sababu kubwa ni kuwa Iniesta hawezi kuwa yule tena kwa nyakati kadhaa kwa sababu nguvu imepungua, lakini pia Neymar hajawa katika kiwango chake kwa muda mrefu ingawa amekuwa muhimu kwa kutoa pasi za mwisho kwenye UEFA, katoa 7. Nguvu ya Rakitic pia imepungua lakini UEFA ni UEFA na Barcelona wamepazoea.

KIUFUNDI

Tatizo kubwa la PSG ni kuamua mchezo kwenye uwanja wa nyumbani. Parc des Princes ni sehemu ambayo kwenye hatua za mtoano wamekuwa wakipata shida kupata ushindi dhidi ya vilabu vikubwa. Na wakati huu ambao watamkosa Thiago Silva wanatiwa kuwa makini zaidi. Nampenda Unai Emery kwenye hatua za mtoano, anajua kuchanga karata.

Jambo zuri kwao linaweza kuwa kurejea kwa Marco Verratti. Huyu anafahamu namna ya kuutumia mpira ukiwa miguuni. Ni ngumu kumzuia na ndiye anayetakiwa kuamua timu itachezaje wakati huu ambao eneo la kiungo la Barceloa halina hatari iliyozoeleka.

Draxler na Moura wanaweza kuwa silaha nyingine ya muhimu kwa sababu mmoja wapo lazima aanzie nje. Hivyo wana uhakika wa kuwa na kasi kwa dakika zote 90, kwa sababu msaada kwa Di Maria utapatikana huku nguvu ya Matuidi ikiwasaidia sana.

BARCELONA

Kwa upande wa Barcelona, kuna Lionel Messi. Mfungaji bora wa UEFA msimu huu, ana mabao 10 mpaka sasa. Huyu ndiye hasa atakuwa anatizamwa zaidi na PSG hasa wakati huu ambao Kimpembe atatakiwa kuziba nafasi ya Thiago Silva kwa PSG. Lakini ili Barcelona wawe na uhuru kwenye mchezo huu ni muhimu Neymar acheze, kwa sababu kasi ya mabeki wa mapembeni wa PSG ni hatari. Serge Aurier na Kurzawa wanaweza kuwa tatizo iwapo upande wowote wa pembeni kwa Barcelona utakosa nguvu.

Lakini akili ya Barcelona itakuwa kwenye miguu ya Andres Iniesta, huyu akicheza kama alivyozoeleka na hivi Enrique alimpa mapumziko wiki hii inakuonyesha ni kwa namna ipi anategemewa kutumika kuamua mchezo huu. Vinginevyo Andre Gomez lazima awe imara.

MAMBO YA KUTEGEMEA

Unaweza kuwa na uhakika kuwa mabao mawili au zaidi yatafungwa. Hii ni kutokana na sababu kuwa timu zote zina silaha za kufunga lakini pia zina udhaifu kwenye eneo la Ulinzi. Huku  PSG ikiwa haijawahi kumaliza mchezo dhidi ya Barcelona bila kuruhusu bao.

Pamoja na PSG kutokujua kumaliza mchezo vyema nyumbani, lakini bado wamefungwa mara moja kati ya 42 nyumbani na hiyo ikiwa dhidi ya Barcelona. Akili ya Suarez ikimaliza mchezo mwaka 2015. Utamu wa mchezo huu ni kuona kama wataendeleza rekodi.

UTABIRI

Suarez atafungaDi Maria atafungaPSG atashinda

Post a Comment

[blogger]

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.