Suluhisho la nguvu za kiume
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.
Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.
Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.
Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).
Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.
Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.
Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:
Umri wakoUtendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuuguaAfya yako kwa ujumlaMatatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.kNini sababu ya wewe kutaka kupona
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.
Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake. Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.
Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke. Sababu nyingine amabzo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
WasiwasiHasiraMsongo wa mawazo (Stress)HuzuniHofu na mashakaKukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:
Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosaMisuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosaKiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:
UzeeKisukariKujichua/PunyetoUzinziKukosa Elimu ya vyakulaKutokujishughulisha na mazoeziShinikizo la juu la damuUgonjwa wa moyoUvutaji sigara/tumbakuUtumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani,Kudhurika kwa neva au uti wa mgongoMadawa ya kulevyaKupungua kwa homoni ya testeroneAthari kutoka kwa baadhi ya dawaPombeNguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Kitu gani husababisha uume usimame?
Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.
Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.
Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya uume. Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Mtazame mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.
Mbegu-za-Maboga
Suluhisho la nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Njia 13 za kujitibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume:
1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna,
2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.
4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.
Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.
5. Tumia kitunguu swaumu
Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja.
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi mbalimbali mwilini.Unafahamu kuwa kitunguu swaumu ni dawa ya zaidi ya magonjwa 30 mwilini?
6. Kula tikiti maji
Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.
Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.
Faida nyingine 12 za tikiti maji kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume
• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.
7. Kula ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.
8. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.
Kama unataka kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu umhimu wa chumvi mwilini,
9. Kunywa maji mengi kila siku
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.
10. Tafuna mbegu za maboga
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo/stress kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya kuliko zote ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.
Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukipiga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga.
NAMNA NZURI YA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA KAMA DAWA:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.
Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga, ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kila siku. Unatafuna na ganda lake hasa kama zimekaangwa tayari
Kwa muda gani? Kwa wiki 3 mpaka 4 kwa ugonjwa wowote kati ya haya niliyoeleza. Kumbuka pia unaweza kutumia mbegu hizi hata kama huumwi chochote!
11. Tumia asali yenye mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake. Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari. Au unaweza kuweka vijiko vikubwa vitatu ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote kutwa mara 2 amabapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini.
12. Kunywa chai ya tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!
13. Tumia unga wa msamitu
Unga wa msamitu (mtishamba wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya uume. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari. Unga huu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama.
Msamitu pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.
Msamitu unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika nguzu za kiume.
Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, Msamitu unapokuja kukutibu unakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.
Kama huhitaji dawa yoyote ila unahitaji kuniona binafsi, weka miadi (appointment) kwa kubonyeza hapa.
Baadhi ya maswali ninayoulizwa mara kwa mara
1. Utajuaje mke au mpenzi wako amefika kileleni?
2. Je, Mwanaume anatakiwa kuwa na uume wa ukubwa gani?
3. Je Kuna Faida au Hasara ya Kupiga Punyeto au Kujichua?
4. Je Mwanamke niliyenaye anaweza kuwa sababu ya mimi kuishiwa nguvu za kiume?
Kama unahitaji kuonana na mimi binafsi, weka miadi (appointment) kwa kubonyeza hapa.
Post a Comment