MTOTO wa Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah bin Abdul Aziz azua gumzo baada ya kusafirisha ndege 80 aina ya mwewe kwa kutumia ndege.
Picha moja katika tovuti ya Reddit iliyotoka jana (Jumatatu) asubuhi, ilizua taharuki kwenye mtandao wa Intanet ambapo ilionyesha ndege 80 waliokuwa wakisafirishwa kwenye ndege wakiwa viti.
Hata hivyo, jambo hilo si la ajabu katika Mashariki ya Kati kuhusiana na kusafirishwa kwa ndege ambao Reddit walisema ni mwewe, lakini wakionekana kuwa ni vipanga.
Usafirishaji wa vipanga katika nchi za Mashariki ya Kati ni jambo la kawaida ambalo limefanywa kwa maelfu ya miaka ikiwa ni pamoja na kuwafundisha ndege hao kuwinda. Ifahamike pia kwamba kipanga ni alama ya taifa ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), hivyo mashirika ya ndege yanayosafiri eneo hilo yanategemewa kutia maanani mahitaji ya ndege hao.
Mtumiaji mmoja wa tovuti ya Reddit amesema katika makala moja kwamba vipanga wanaweza kupewa pasipoti kutoka UAE na kuweza kusafiri kwenda Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, Pakistan, Morocco na Syria. Hiyo ni kwa mujibu wa makala hiyo ambayo imeongeza kwamba pasipoti hiyo huwa inatumika kwa miaka mitatu.
Mwakilishi wa shirika la ndege la Flydubai alimwambia Frank Kane, mwandishi wa tovuti ya UAE ya ‘The National’, kwmba vipanga lazima wawe na viti vyao kwenye ndege na kufungwa vitambaa maalum kuwaepusha na matukio ya ajali.
Vilevile, kwa mujibu wa mwandishi huyo, daraja maalum kwenye ndege (business class) la Flydubai mnamo Aprili 2015 lilitengwa maalum kwa vipanga, hivyo kufanya tukio hilo kuwa si la ajabu.
Katika daraja la kawaida la shirika la ndege la Qatar , mtu anaruhusiwa kusafirisha vipanga wasiozidi sita, hii pia inaruhusiwa katika shirika la ndege la Etihad.
Post a Comment