Na nyalusiblog
IMESIMULIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI………….0744 000 473
Wachawi wana uwezo wa kutengeneza magonjwa mbalimbali kama vile ugumba, udhaifu wa nguvu za kiume, kifafa, upofu, ukichaa, kiharusi, ukimwi nakadhalika.
Hapa mgonjwa akienda kupimwa hospitali anakutwa hana tatizo wala ugonjwa wowote lakini anakuwa anaonyesha dalili zote za ugonjwa husika. Ukiona hali hiyo basi ujue ugonjwa wako umetengenezwa na wachawi.
Mara nyingi,ingawa si mara zote, kabla wachawi hawajamtupia mtu ugonjwa husika, hujidhihirisha kwanza kwa kutumia njia zao za kichawi kama muhusika hana maradhi wanayo taka kumsababishia.
Kama wakigundua mhusika tayari anaugua maradhi wanayo taka kumsababishia, basi humtengenezea ugonjwa mwengine, na ndumba ambazo zingetumika kumsababishia maradhi mhusika, huelekezwa kwa mtu mwingine ( Katika ulimwengu wa wachawi, ndumba zina gharama kubwa sana, hivyo huwa hazitumiki bila sababu wala faida )
Kwa mfano huko vijijini, kama wachawi wanataka kumtengenezea mtu ugonjwa wa kisukari, watataka kwanza wajue kama mtu huyo tayari ana maradhi ya kisukari au bado hajaanza kushambuliwa na kisukari.
WACHAWI WANAJUAJE KAMA MTU FULANI ANA MARADHI YA KISUKARI
Kujua kama mtu Fulani ana maradhi ya kisukari, wachawi watafuatilia mienendo ya mtu huyo kwa lengo la kupata sehemu atakayo kojoa. Siku wakibahatisha kumuona mhusika amekojoa mahali, basi watakwenda hadi kwenye eneo alipokojoa na kusubiri kwa muda wa kuanzia dakika arobaini hadi lisaa limoja. Ndani ya muda huo, KAMA WATATOKEA SISIMIZI, basi ujue mtu huyo ANA KISUKARI lakini KAMA SISIMIZI HAWATATOKEA basi ujue mtu huyo HANA MARADHI YA KISUKARI. Baada ya kipimo hicho ndipo watachukua hatua stahiki, za ama kumsababishia maradhi ya kisukari ama vinginevyo ( KUHUSU NAMNA WACHAWI WANAVYO TENGENEZA “KISUKARI CHA KICHAWI” NITAELEZEA SIKU ZIJAZO.)
Ukimwi wa Kichawi : Katika ulimwengu wa kitabibu, “ ukimwi wa kichawi” ni pale mtu anapo onyesha dalili zote za muathirika wa ukimwi, lakini vipimo vya hospitali vinaonyesha mtu huyo yupo ( HIV-NEGATIVE) yaani bado hajaathirika .
Hapa mgonjwa husika, atapimwa vipimo vyote vya hospitali na vyoote vitaonyesha hajaathirika, lakini ataendelea kuonyesha dalili zote za mgonjwa wa ukimwi . Mgonjwa huyu ataendelea kuugua na kuteseka bila kupata nafuu yoyote licha kutumia dawa mbalimbali, na mwisho wa siku atapoteza maisha yake.
Zipo njia kuu mbili wanazo tumia wachawi kusababisha maradhi ya aina mbalimbali kwa watu mbalimbali. Njia ya kwanza, ni kwa njia ya kuwalisha dawa mbalimbali za kichawi, ambazo husababisha maradhi ya aina mbalimbali ( WACHAWI WANA MAARIFA MAKUBWA SANA JUU YA MITI MBALIMBALI INAYO SABABISHA MARADHI NA MATATIZO MBALIMBALI )
Njia ya pili ni kwa njia ya majini. Hapa mgonjwa husika, atasababishiwa maradhi ya aina Fulani kwa kutumiwa majini majini ambayo yameapishwa kwenda kufanya makazi yao kwenye damu ya mtu aliekusudiwa na kusababisha maradhi Fulani kwa mtu huyo, hadi pale umauti utakapo mkuta.
Katika kutengeneza “ ukimwi wa kichawi “ pia zipo njia kuu mbili zinazo tumiwa na wachawi. Njia ya kumlisha mkusudiwa ndumba za kichawi ambazo husababisha mtu kuugua maradhi yanayo fanana dalili zake na maradhi ya ukimwi na njia ya pili ni kumtupia majini ambayo yatamfanya augue maradhi yanayo fanana na ukimwi.
Leo tutaangalia njia ya kwanza, yaani njia ya kumlisha ndumba za kichawi mtu aliye kusudiwa. Tutaangalia njia wachawi wanavyo weza kumlisha mtu uchawi, utakao msababishia maradhi ya ukimwi na jinsi unavyo weza kujikinga dhidi ya husda hiyo, na kwa wale ambao tayari wameshalishwa uchawi huo, jinsi wanavyo weza kusaidiwa kupata tiba ya kuondoa maradhi hayo ya kichawi mwilini.
Zipo njia zaidi ya arobaini ambazo wachawi wanaweza kuzitumia, kutengeneza uchawi na kumlisha mtu, ambao utamsababishia kuugua maradhi ambayo dalili zake zinafanana na ukimwi. Leo tutaingalia njia moja wapo kama ifuatavyo
JINSI WACHAWI WANAVYO TUMIA MAJI YA KISIMA KUTENGENEZA “ UKIMWI WA KICHAWI “
Awali ya yote, wote tunapaswa kufahamu kwamba katika ulimwengu wa tiba za jadi “ MAJI” yanaweza kutumika kama TIBA na wakati huo huo, yanaweza kutumika kama “ UCHAWI WENYE KUDHURU”
Maji yenyewe kama yenyewe, bila kuchanganya na kitu chochote kile, yanaweza kutumika kama tiba ya magonjwa karibu yoote unayo yafahamu, kuanzia kisukari, kifafa, ugumba, udhaifu katika nguvu za kiume, kuongeza urefu wa maumbile ya kiume ( HAPA HUTUMIKA MAJI YAITWAYO MAJI YA FATIRU ), fangasi za sehemu za siri, magonjwa ya ngozi, nakadhalika.
Sio tu katika kutibu magonjwa na maradhi mbalimbali, maji pia hutumika kama tiba dhidi ya matatizo mbalimbali ya kimaisha kama vile kuondoa nuksi, mikosi nakadhalika.
Vile vile maji yanaweza kutumika katika kutengeneza uchawi wenye kudhuru, wa aina mbalimbali.
( KATIKA SIKU ZINAZO KUJA, NITAWEKA SOMO KUHUSU TIBA MBALIMBALI ZA JADI KWA NJIA YA MAJI BILA KUSAHAU, JINSI WACHAWI WANAVYO TUMIA MAJI KUTENGENEZA UCHAWI WENYE KUDHURU WA AINA MBALIMBALI )
Katika ulimwengu wa tiba za jadi, maji ya mtoni, baharini, ziwani, kisimani, kwenye dimbwi nakadhalika, huweza kutumika eidha kama tiba ya magonjwa mbalimbali au kama uchawi wa aina mbalimbali.
Kinacho yapa maji hayo kuwa na nguvu ya kitabibu, ni njia zilizo tumika kuyachukua maji hayo. Kila maji yanatumika katika tiba yake na uchawi wake. Maji ya mtoni yana tiba zake na uchawi wake, maji ya ziwani, maji ya baharini, kisimani nakadhalika.
Mfano mdogo, maji ya mtoni yanaweza kutumika katika kutengeneza uchawi unaoitwa “ NSUNKWA” ambao ni maalumu kwa ajili ya kumuhamisha adui yako, aende kuishi mbali na wewe.
Kila aina ya maji yana taratibu yake namna ya kuyachukua na kuyatumia katika eidha tiba au uchawi.
Leo tutaona jinsi wachawi wanavyo tumia maji ya kisima, katika kutengeneza maradhi ya ukimwi.
Katika kutengeneza ukimwi wa kichawi, wachawi hufanya kama ifuatavyo :
Kwanza wanachukua maji ya kisima kisicho kauka .Pili wanachukua kitovu cha mtoto mchanga kilichodondoka chenyewe ( Kuweni makini sana na vitovu vya watoto wenu )
Tatu wanachukua “ Tegelo” ; Kwa wale wasio fahamu Tegelo ni mfuko wa chakula cha kuku na chakula chake. Tegelo na kitovu cha mtoto, vinachanganywa na dawa zingine za aina kumi na tatu ( sitazitaja zote kwa sababu za kimiiko ya kazi yangu: kuna watu wabaya wanaweza kujifunza kitu hapo na kwenda kuwaumiza watu )
Vikishachanganywa vinachomwa vyote kwa pamoja, kisha vinaenda kupikwa njia panda usiku wa manane kwenye hayo maji ya kisima, pamoja na mafuta ya usiku. Baada ya hapo linafanyika tambiko maalumu kisha vitu hivyo vinaenda kuzikwa kaburini kwa muda wa siku saba. Baada ya hapo uchawi huo utakuwa umekamilika.
JINSI WANAVYO TEGA UCHAWI HUO : Uchawi huo hupitia kwenye chakula ( sana sana “ mboga yenye mchuzi “), au kinywaji.
Mtu atakae lishwa uchawi huu ataanza kuonyesha dalili za ugonjwa wa ukimwi, kulingana na muda alio nuiziwa, kama amenuiziwa aanze kuugua baada ya miezi sita, basi baada ya miezi sita kweli ataanza kuugua maradhi hayo, kama ni mwezi mmoja ni mwezi mmoja.
Mkilishwa mke na mume, basi mke na mume wote mtaugua maradhi hayo. Mkilishwa familia nzima, basi familia yote mtaugua maradhi hayo mmoja baada ya mwingine. Ndio maana baadhi ya familia unakuta watu wote ni waathirika.
Na kama mtalishwa kwenye sherehe , au msiba, basi watu wote mtaugua maradhi ya ukimwi, isipokuwa tu wale wenye kinga zao.
TIBA YAKE.
Zipo tiba za aina nyingi ambazo zinatibu maradhi haya ya kutengenezwa. Leo tutaangazia tiba moja wapo.
Kama una muuguza mgonjwa ameugua maradhi haya kwa muda mrefu, bila nafuu yoyote. Ameenda kupima hospitali akaambiwa hajaathirika lakini bado anaendelea kuonyesha dalili za mtu aliye athirika, basi fanya kama ifuatavyo:
==>Moja chukua dawa inaitwa Mlali, pili chukua dawa inaitwa Hangachalo,. Tatu chukua dawa inaitwa Tarigula, Nne chukua dawa inaitwa Mwinula, Tano; chukua dawa inaitwa Mzima
==>Dawa hizi zitachemshwa pamoja na kisu kikiwa kimesimama ndani, kisha unampa mgonjwa wako anakuwa anakunywa mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni kwa siku thelathini., Na nyingine unakuwa unampiga nayo mgongoni kila anapokuwa anakunywa.
Atatapika uchawi wote,na ndani ya siku arobaini, inshaalah uchawi na sumu yote itakuwa imetoka mwilini na atarejea katika hali yake ya kawaida.
KINGA : Kinga ni bora, kuliko tiba. Kujiepusha na shari kama hii, unatakiwa uwe na kinga bora.
Zipo kinga nyingi bora, ila leo nitaelezea kuhusu kinga moja. Kinga hii inatengenezwa kwa mchanganyiko wa miti na vizimba zaidi ya mia moja na ishirini . Moja kati ya vizimba vilivyopo katika kinga hii, ni mti mmoja ambao haupatikani popote pale duniani isipokuwa mkoa wa Kigoma tu.
Ukiwa na kinga hiyo, na ikatokea umelishwa uchawi wa aina yoyote ile utautapika, na aliye kuwekea uchawi huo, atapata madhara makubwa.
Post a Comment