Ukawa ‘watifuana’ uchaguzi mdogo Sengerema

Sengerema. Wakati uchaguzi mdogo kujaza nafasi zilizo wazi za udiwani na Jimbo la Dimani lililopo Zanzibar unatarajia kufanyika Januari 22, 2017, mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya CUF umeauthiri Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wilayani hapa.

Vyama vikubwa katika Ukawa vya Chadema na CUF kila kimoja kimeamua kusimamisha mgombea katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kahumulumo.

Katika makubaliano ya vyama hivyo wakati vinaanzisha umoja huo, miongoni mwa mambo viliyoafikiana ni kuachiana majimbo, kata na vitongoji kwa vyama vinavyokubalika katika maeneo husika.

Akizungumzia kutoshirikiana na CUF, Katibu wa Chadema Jimbo la Sengerema, Deusdedit Mwigala alisema juhudi za kusimamisha mgombea mmoja zilikwamishwa na msimamo wa CUF wa kusimamisha mgombea wao.

“Tuliwafuata wenzetu wa CUF kuomba tushirikiane kusimamisha mgombea mmoja, lakini walikataa wakisema nao watasimamisha mgombea wao,” alisema.

Katibu wa CUF Wilaya ya Sengerema, Yusuph Ihovelo alisema chama hicho kimeamua kusimamisha mgombea baada ya kupokea maelekezo kutoka uongozi wa juu.

Kutokana na mgogoro uliopo upande wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ulikuwa unasubiri uamuzi wa Ukawa, lakini ule wa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba uliahidi kusimamisha mgombea katika kata zote zilizo wazi.

Uamuzi huo umeonekana kuifurahisha CCM ambayo kupitia Katibu wake wa wilaya, Solomon Kasaba ametamba kuibuka na ushindi katika uchaguzi kwa madai kuwa vyama hivyo vitagawana kura.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kahumulo ambaye pia ni Mtendaji wa kata hiyo, Kepha Chima alisema vyama hivyo viwili nimewasilisha majina ya wagombea na wote wamepitishwa kuwania nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo, wagombea hao wa Chadema na CUf watachuana na mwenzao wa CCM katika uchaguzi huo baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Joseph Kando maarufu kwa jina la Njiwapori kujiuzulu.

Aliwataja wagombea waliopitishwa na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Fotunatus Nzwagi (CCM), Doto John (Chadema) na Ntalikwa Ishatala wa CUF.

“Wagombea wote wametimiza vigezo na masharti yote kuanzia kujaza fomu na kuzirejesha kwa muda mwafaka na hawajawekewa pingamizi,” alisema Chima.

Post a Comment

[blogger]

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.