Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan
Makubaliano ya kusitishwa mapigano kote nchini Syria yameanza kutekelezwa.
Mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi, yamesitishwa kwingi lakini kuna ripoti kuwa yanaendelea kwa kiwango kidogo katika sehemu chache tu.
Hii ni kwa sababu makundi mengine hayajashirikishwa kwenye makubaliano hayo ya amani na mapambano bado yanaendelea dhidi la makundi ya Nusra Front, YPG , na vilevile lile la IS .
Makubaliano hayo yaliafikiwa kwa ushirikiano wa Urusi na Uturuki yakiungwa mkono na Iran, lakini Marekani haikuhusishwa.
Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan katika kipindi cha mwezi mmoja.
Rais Bashar al-Assad amekubali kuteeleza makubaliano hayo
Shirika la wachunguzi wa haki za kibinaadamu nchini Syria SOHR ,lenye makao yake huko Uingereza limesema kuwa maeneo mengi ya taifa hilo yalikuwa yametulia usiku kucha.
Lakini limeripoti vita vikali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Hama.
Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman ameiambia AFP: makundi madogo ya waasi
pamoja na makundi yanayotii waasi hao yanajaribu kuharibu makubaliano hayo kwa sababu mpango huo unapuuzilia mbali uwepo wao.
Post a Comment