Ofisi za Shirika la Umeme ( Tanesco)
Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa mwaka mpya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) amekubali maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza bei ya umeme.
TANESCO waliomba kuongeza umeme kwa asilimia 18.9 lakini baada ya EWURA kufanya mchakato wamekubali ombi la kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 8.5 kuanzia mwezi January 2017.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa asilimia hizo 8.5 zitakazo ongezeka kuanzia mwezi January 2017 hazita wagusa watumiaji wa umeme ambao matumizi yao hayazidi Unit 75 kwa mwezi.
Post a Comment