December 2016

Na nyalusiblog

 Watu wawili wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya National Express T.662 DEF, baada ya kuacha barabara na kupinduka zaidi ya mara tatu katika eneo la kijiji cha Tumuli, wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Waliofariki ni dereva wa basi hilo Athumani Idd (47) mkazi wa Mabibo jijini Dares Salaam na mwalimu wa shule ya msingi Malunga aliyefahamika kwa jina moja la Janet (anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 29).

Habari zilizopatikana jana eneo la tukio, zimedai kuwa katika siku za hivi karibuni mwalimu Janet alimpeleka mama yake jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Imedaiwa kuwa baada ya kufika Dar es Salaam, aligundua kuwa amesahau kuchukua kadi ya bima ya afya, na hivyo akalazimika kurudi Iramba.

Jana asubuhi Janet alichelewa basi la National Express katika kituo cha Kyengenge na kuamua kukodi bodaboda kulifukuzia basi hilo na kufanikiwa kulikuta kituo cha Malunga. Baada kupanda basi hilo, dakika chake baadae, basi hilo lilipata ajali na kulaliwa na basi kichwani.

Watu hao wamefariki dunia papo hapo na miili yao ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida. Basi hilo lilikuwa linatokea New Kiomboi, likielekea jijini Dar.

Akizungumza kwenye eneo la tukio, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida , ACP Debora Daudi Magiligimba, alisema ajali hiyo imetokea Desemba, 30 saa 12.45 asubuhi katika eneo la kijiji cha Tumuli.

Alisema ajali hiyo pia imesababisha majeruhi 26 ambao wamelazwa katika hosipitali ya mkoa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kamanda Magiligimba alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na mwendo kasi na uzembe.

“Eneo hili ilipotokea ajali hii kuna mteremko na kona kali. Kutokana na mwendo kasi, dereva alishindwa kulimudu na hivyo kuacha barabara na kuingia kwenye korogo la mto, na kuruka juu kisha kupinduka mara tatu,” alisema.

Kwa upande wake mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk. John Mwombeki, alikiri kupokea miili ya watu wawili waliofariki dunia kwenye ajali ya basi la National Express, pamoja na majeruhi 26.

“Kati ya majeruhi hawa, mmoja dada Joyce tumempa rufaa kwenda hospitali ya taifa Muhimbili kutokana na sehemu yake ya mwili ya chini kutokufanya kazi. Majeruhi 10 wao tunaendelea kuwafanyia uchunguzi” alisema Dk. Mwombeki.

Mmoja wa majeruhi hao mfanyakazi wa shirika la TBC jijini Dar es Salaam, Victor Elia, alisema pamoja na kupoteza kila kitu, anamshukuru Mungu kwa kupona kufa kwenye ajali hiyo mbaya.

“Kilichonisaidia ni kufunga mkanda … abiria wenzangu wote ambao hawakufunga mikanda ndio walioumia zaidi wakiwemo waliopoteza maisha. Ajali hii kwa vyovyote imechangiwa na mwendo kasi,” alisema Victor ambaye ni mtayarishaji na mtangazaji wa TBC.

Kondakta wa basi hiyo, Nicolaus Apolinari (23) mkazi wa jijini Dar es Salaam, alisema ajali hiyo imechangiwa na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.




 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti mgema akionyesha moja ya sehemu ambayo moto bado unawaka.

 Hivi ndivyo hali halisi ya ofisi ilivyoungua kwa ndani

 Nyaraka za serikali ya kijiji cha Mtyangimbole zikiwa zimeteketea kwa moto na kubaki majivu


Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgemaakizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtyangimbole  baada ya zoezi la kuzima moto kumalizika. Kwa undani wa habari hii angalia hiyo video.

(Habari na RUVUMA TV)



Kesi ya wizi wa simu aina ya Tecno iliyochukua takriban miaka miwili mahakamani, imefika tamati kwa mtuhumiwa kufungwa maisha jela. 

Hukumu hiyo ilifikiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya mtuhumiwa Kassim Salum (18) kukutwa na hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu wa simu yenye thamani ya Sh110,000. 

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 28, mwaka jana katika Mtaa wa Ghana Magenge eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam. 

Ushahidi uliotolewa na mashahidi watano uliiwezesha mahakama kukubaliana na madai ya mlalamikaji Lutifia Mohamed. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule alisema, “Baada ya kusikiliza mashahidi wote watano wa upande wa jamhuri, mahakama inaona wamethibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.” 

Akipitia ushahidi huo, hakimu Haule alisema mshtakiwa alimsukuma mlalamikaji na kuangukia katika karai la mafuta ambalo lilikuwa jikoni. 

Mashahidi hao waliieleza jinsi mshtakiwa alivyomvamia mlalamikaji akimtaka atoe simu aliyokuwa nayo na katika purukushani hizo, alimpiga ngumi tumboni hali iliyosababisha kuishiwa nguvu. 

Ilielezwa kuwa kutokana na kupigwa, mlalamikaji aliirusha simu upande wa pili ambapo kulikuwa na muuza chipsi, hivyo Salum aliamua kumuachia mlalamikaji ili aende kuifuata. 

Hata hivyo, wakati mlalamikaji anajaribu kuokota simu yake, Salum alimsukuma akaangukia katika karai la mafuta ya moto na kumsababishia kuungua eneo lote la mgongoni. Inadaiwa baada ya hapo Salum alichukua simu hiyo na kutoweka nayo. 

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliomba mahakama impe adhabu kali Salum ili aweze kujifunza kwa kuwa amemtia mlalamikaji ulemavu wa kudumu. 

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea na Salum aliomba isimpe adhabu kali akisema si yeye aliyechukua simu hiyo, bali ni chuki binafsi za mitaani wanakoishi. 

JESHI la Polisi Manyara linamshikilia mtu mmoja kwa kusafirisha misokoto 447 ya bangi, ambayo alihifadhi kwenye ndoo na kuweka juu ya unga wa sembe ili kupoteza ushahidi wa kufahamika kwa bangi hiyo.

Kamanda wa Polisi Francis Massawe, jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakati maaskari walipokua doria ndipo walipomtia nguvuni mtuhumiwa.

“Mtu huyo alikamatwa Desemba 27, wakati askari walipokuwa kwenye misako na operesheni za kawaida huko katika kata ya Bonga akiwa ndani ya gari namba T.912 BFA lililokuwa likitokea Arusha kuelekea Kondoa,’’ alisema Massawe.

Kamanda Massawe hakumtaja majina kwa sababu za kiuchunguzi ila alidai anaumri wa miaka (35) ni mwanaume kutoka kijiji cha Mwongozo, kilichopo wilaya ya Kondoa vijijini.

Massawe alisema basi alilokuwa amepanda ni aina ya Nissan, ila halikuweza kujulikana la kampuni gani kwa kuwa lilikuwa halijaandikwa jina lolote.

Source: Nipashe

 MC Pilipili akiwa na Rose Ndauka katika moja ya onyesho lake lililofanyika Dodoma weekend hii

Baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa mchekeshaji MC Pilipili anatoka kimapeniz na Rose Ndauka, muigizaji huyo amekanusha uvumi huo.

Wiki chache zilizopita kupitia kipindi cha The Play List cha Times FM mchekeshaji huyo alidaiwa kukiri kutoka kimapenzi na muigizaji huyo.

Ijumaa hii muigizaji huyo amescreenshot ujumbe wa mtangazaji wa The Play List, Lilommy ambao ulidai huwenda wawili hao wakawa wanatoka kimapenzi na kuandaika

“Jamaniii naomba niweke ili swala sawa sawa, mimi na MC Pilipili ni watu tunaofahamiana haswa kwenye kazi hatuna uhusiano wowote wa kimapenzi. NADHANI NTAKUWA NIMEELEWEKA”



Ofisi za Shirika la Umeme ( Tanesco)

Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa mwaka mpya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) amekubali maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza bei ya umeme.

TANESCO waliomba kuongeza umeme kwa asilimia 18.9 lakini baada ya EWURA kufanya mchakato wamekubali ombi la kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 8.5 kuanzia mwezi January 2017.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa asilimia hizo 8.5 zitakazo ongezeka kuanzia mwezi January 2017 hazita wagusa watumiaji wa umeme ambao matumizi yao hayazidi Unit 75 kwa mwezi.

Rapper Chemical amedai kauli yake ya kuwa yeye bado ni bikira (bado hajaupoteza usichana wake) umewafanya wanaume wengi kumtokea huku watu wengine wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.

Chemical amedai wakati anatoa kauli hiyo hakudhamiria kuweka wazi suala hilo lakini alilazimika kutoa jibu hilo baada ya kuulizwa swali.

“Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine wanasema sikuwa na busara kufanya vile,” Chemical alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Lakini nataka kuwaambia kwanza sikujitangaza ila ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana siwezi kuvijibu,”

Aliongeza, “Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo, mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye ‘Career’ yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae kuniharibia maisha yangu” alisema Chemical

Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza kutaka kumtafutia mwanaume na kusema yeye hana shida hata wakimtafutia mwisho wa siku yeye lazima ampime kuona kama anamfaa au hafai.



 Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan

Makubaliano ya kusitishwa mapigano kote nchini Syria yameanza kutekelezwa.

Mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi, yamesitishwa kwingi lakini kuna ripoti kuwa yanaendelea kwa kiwango kidogo katika sehemu chache tu.

Hii ni kwa sababu makundi mengine hayajashirikishwa kwenye makubaliano hayo ya amani na mapambano bado yanaendelea dhidi la makundi ya Nusra Front, YPG , na vilevile lile la IS .

Makubaliano hayo yaliafikiwa kwa ushirikiano wa Urusi na Uturuki yakiungwa mkono na Iran, lakini Marekani haikuhusishwa.

Iwapo mpango huo utafanikiwa licha ya visa vichache vya ghasia ,mazungumzo ya amani yataanza kufanyika nchini Kazakhstan katika kipindi cha mwezi mmoja.

Rais Bashar al-Assad amekubali kuteeleza makubaliano hayo

Shirika la wachunguzi wa haki za kibinaadamu nchini Syria SOHR ,lenye makao yake huko Uingereza limesema kuwa maeneo mengi ya taifa hilo yalikuwa yametulia usiku kucha.

Lakini limeripoti vita vikali kati ya wanajeshi wa serikali na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Hama.

Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman ameiambia AFP: makundi madogo ya waasi

pamoja na makundi yanayotii waasi hao yanajaribu kuharibu makubaliano hayo kwa sababu mpango huo unapuuzilia mbali uwepo wao.

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.