Na Ezekiel Nyalusi
Hatimae robo fainali ya michuano ya Champions leauge imewekwa hadharani,baada ya timu 8 kufudhu sasa zitapambana kwenye wiki ya tarehe 10 April ili kutafuta timu zitakazocheza nusu fainali ya champions league.
Mabingwa watetezj wa ligi kuu Uingereza timu ya Leicester City baada ya kuwatoa Valencia sasa watapambana na Athletico Madrid,Athletico wana njaaa na ubingwa safari hii baada ya kupoteza katika fainali iliyopita ya Champions League.Leicester hii sio mara yao ya kwanza kukutana na Athletico kwani wameshakutana mara mbili hapo kabla ikiwa ni mwaka 1962 na 1998 huku Leicester akipoteza michezo yote miwili.
Miamba ya Ujerumani Borrusia Dortmund nao watakuwa wenyeji wa Monaco ambao waliitoa Man City katika mechi za 16 bora.Dortmund wenyewe walifudhu katika hatua hii baada ya kuwatupa nje klabu ya Benfica ya Ureno.
Mechi kali itakayovuta hisia za watu ni kati ya mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich ambao watacheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya klabu ya Beyern Munich.Achana na hiyo sasa kwani ni kama mkosi kwa Dani Alves ambaye alisema hatamani wakutane na Barcelona lakini imetokea kwani Juventus wanakutana na Barcelona,mechi hii ni kama kumbukumbu ya robo fainali ya champions league mwaka 2015 ambapo Barcelona waliibuka kidedea dhidi ya Juventus
Post a Comment