Kuishi karne moja au zaidi duniani ni mafanikio makubwa katika maisha ya binadamu lakini kutokana na kuongezeka sababu zinazopelekea mtu kufa mapema ikiwemo hali ngumu ya maisha na kukosa furaha na amani, imeelezwa kuwa ili uishi muda mrefu ni lazima ufanikiwe katika afya.
Wapo watu waliowahi kuishi miaka 100 na zaidi na wengine wapo hata sasa huku wengi wakiwa na siri za kuishi muda mrefu kiasi hicho.Mtandao wa indiatime.com kwa msaada wa watu walioishi kwa miaka mingi duniani umezitaja siri 7 ambazo zikizingatiwa zinaweza kumfanya mtu akaishi kwa muda mrefu zaidi.
1: Kutembea sana kwa miguu
George Boggess hakufikisha miaka 105 lakini aliishi zaidi ya miaka 100 aliwahi kutoa ushauri na siri ya kuishi umri mrefu kuwa ni kutembea.
2: Kula samaki na kulala kwa angalau saa 8
Misao Okawa, ambaye alitambulika kama binadamu mwenye umri mkubwa zaidi dunia ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 117 alisema sushi (samaki) na saa 8 za kulala ni siri ya kuishi kwa muda mrefu.
Wajapan wanatajwa kuwa na uwiano wa kuishi muda mrefu ambapo kuna zaidi ya watu 5,000 wanaosemwa kuishi zaidi ya mika 100.
3: Kupiga push-ups tano hadi saba kila siku
Duranord Veillalord ambaye alitimiza miaka 109 mwaka jana anaianza siku yake kwa pushups kila siku. Pushups, kikombe cha chai na matunda ni siri ya kuishi kwa miaka mingi.
4: Kaa mbali na vipodozi
Adelina Domingues alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi Marekani ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 114 anasema siri kubwa ya yeye kuishi miaka mingi ni kujiweka mbali na vipodozi.
5: Kunywa uji wakati wa kufungua kinywa
Jesse Gallan aliishi kwa miaka 109 na kusema siri kubwa ilikuwa kunywa uji kama kifungua kinywa chake pia alisema kutokuwa na wanaume wengi kwenye maisha yake kuliongeza miaka ya maisha yake.
6: Kaa mbali na pombe/ulevi
Alexander Imich wa New York City ambaye aliishi kwa miaka 111 alisema siri kubwa ya yeye kuishi miaka 111 ni kwa sababu alijiweka mbali na kilevi na alikuwa muogeleaji na kufanya mazoezi. Chakula chake kilikuwa ni kuku na samaki na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za kiafya.
7: Kula kwa kiasi
Wanawake wa jamii ya Hunza inayopatikana katika mipaka ya Kashmir, China na Afghanistan hupata watoto wakiwa na miaka 60 na wanaume wanaoonekana kama wana miaka 40. Wazee wa jamii hii wamefikisha umri wa miaka mia moja na wangali na muonekano kana kwamba wana miaka 70 ambapo wanajamii hiyo wakisema siri ni kula kwa kiasi. Wanakula nyama kidogo katika milo miwili kwa siku.
Post a Comment