Mbinu ya urutubishaji mayai IFV
Mtoto mmoja amezaliwa kutoka kwa wazazi walio tasa nchini Ukraine kwa kutumia mbegu za watu watatu.
Madaktari mjini Kiev walitumia mbinu ya kuhamisha seli ikiwa ni mara ya kwanza kwa hilo kufanyika.
Hatahivyo sio mwana wa kwanza aliyezaliwa na jeni za wazazi watatu.
Mtoto huyo wa kike aliyezaliwa mwezi Januari 5 anadaiwa kuwa mtoto wa kisasa mwenye wazazi 3 huku mtoto mwengine akitengezwa kwa kutumia mbinu tofauti kama hiyo nchini Mexico mwaka uliopita.
Kundi hilo la madaktari kutoka Kiev lilirutubisha yai la mama na lile la mpenziwe.
Baadaye walihamisha jeni hizo hadi katika yai lililotolewa na mfadhili.
Hivi ndivyo urutubishaji huo unavyofanyika
Mtoto huyo ana jeni za wazazi wake pamoja na jeni zengine chache kutoka kwa mwanamke wa pili.
Madaktari walianzisha urutubishaji wa mayai ilinkuwasaidia wanawake ambao wako katika hatari ya kuwapatia jeni zenye magonjwa mabaya wana wao.
Mayai kutoka kwa mama mwenye afya mbaya na mfadhili mwenye jeni zenye afya nzuri hukusanywa.
Kliniki ya Nadiya iliopo mjini Kiev ilitumia mbinu hiyo ili kuwatibu wazazi tasa.
Post a Comment