Nyalusi blog
makala iliyopita nilizungumzia madhara ya unywaji wa pombe na kama hukuipata makala hiyo basi isome hapa........, watu wengi ambao ni walevi sana kwenye jamii hudharauliwa na kulaumiwa sana kwa kuendekeza tabia hizo, ni kweli wanaweza kua wanapaswa kulaumiwa lakini upande wa pili ni kwamba watu hawa pia hawapendi kua hivyo na wanashindwa kuacha kwasababu pombe ina kitu kinaitwa addiction yaani mazoea na sio rahisi kuacha kirahisi kwani mwili umeshazoea na unataka zaidi, ikitokea umeacha ghafla hata shughuli zako zitakushinda kwani utapata dalili kitaalamu kama withdraw syndrome ambazo ni kutetemeka, kichwa kuuma, kutapika , kushindwa kula na kua mgonjwa muda wote.
maana yangu ni kwamba mlevi aonekane kama mgonjwa kwenye jamii na kama anataka kuacha pombe basi mpeni msaada na sio kumtenga, swala la kuacha pombe linawezekana kabisa kwa walevi waliopindukia au watu wanaokunywa kawaida tu. yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kuacha pombe..
amua kutoka moyoni; hakikisha maamuzi haya yametoka moyoni mwako kulingana na wewe unavyoona na sio kwamba unataka ili kuacha kuridhisha kikundi fulani au mtu fulani, hii itakupa nguvu ya kupambana na majaribu ya kutaka kunywa pombe tena.
wajulishe wanywaji wenzako nia yako; waambie rafiki zako kwamba umeamua kuacha pombe kwa muda fulani, wape sababu zako za msingi na kama huna waambie ni sababu binafsi za kifamilia, wajulishe kwamba inaweza kua ngumu na utaomba msaada wao iwapo ukiwaka tamaa ya kunywa pombe tena.
jiwekee malengo mafupi; anza kwa kujiwekea kwamba sitakunywa pombe mwezi huu wote wa kwanza, ukifanikisha ongeza mwezi mwingine...hii itakuapa motisha ya kuendelea kuacha kuliko kusema kwanzia leo sinywi tena kwani utajikuta unakunywa. kama mwezi ukiisha na kujikuta umesevu pesa nyingi kwa kutokunywa basi jinunulie zawadi yeyote.
pangilia starehe zako; kama starehe zako nyingi zinahusisha kunywa pombe basi pangilia starehe zingine ambazo hazitaki pombe mfano kwenda bichi, kwenda kuangalia sinema, kungalia mpira uwanjani na kadhalika. epuka kwenda disko na bar kwa kipindi hiki cha mwanzo.
jitoe nje ya raundi za pombe; kama umeacha pombe usijihusishe na kuwanunulia watu pombe kwa kuzungusha kama wanywaji wanavyofanyiana wakiwa bar, nunua kinywaji chako kimoja kama ni soda au juisi kisha kaa pembeni ukinywa. kuwanunulia watu utajikuta na wewe unanunuliwa pombe.
kama mnatoka kwenda kwenye starehe basi endesha gari;kuendesha gari ni sababu kubwa ya wewe kutokunywa pombe kama sheria inavyotaka na hata ukilazimishwa kunywa utawaambia rafiki zako kwamba mimi ni dereva leo.
kua tayari kuzungumzia swala lako; watu wengi watakua wanakuuliza kwanini umeamua kuacha pombe, basi andaa sababu za msingi za kuwaambia kama jinsi pombe inavyoharibu maisha yako ya kijamii, kiuchumi na kiafya na wakati mwingine ukiona umezidiwa waambie ni sababu za kifamilia zaidi.
badilisha sehemu za kukutana na watu; kama ulikua ukipanga kuonana na mtu, unaenda bar basi badilisha sehemu ili ue unaenda kuonana nao kwenye mgahawa au sehemu zingine za wazi ambapo pombe haziuzwi.
furahia faida za kuacha kwa muda huo; angalia ni kaisi gani cha fedha umesevu kwa kuacha pombe, unajisikiaje kukaa muda mrefu bila kupata hangover, unajisikiaje jamii iliyokudharau sasa inakuheshimu na hii itakupa nguvu zaidi a kusonga mbele.
dawa za kuacha pombe kwa walevi sana; kuna dawa maalumu ambazo zimetengenezwa kuwatibu watu ambao wanataka kuacha pombe hasa wale ambao wameshindwa kuacha kwa njia nilizotaja hapo juu, utaratibu huu hufanyika chini ya uangalizi wa daktari hasa kwa nchi zilizoendelea...dawa hizi hufanya kazi kwa kukosesha mtu hamu ya kunywa pombe, kuongeza muda wa hangover mpaka siku tatu, na kuzuia madhara mtu anayopata kwa kuacha pombe haraka mfano disulfiram.[sina uhakika kama zinapatikana nchini], pia unawea kutumia virutubisho mbalimbali vya kuondoa sumu mwilini baada ya kuacha pombe, hivyo unaweza kuvipata hapa nchini.
Post a Comment