January 2017

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi kuitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa, wanasheria na wanasiasa kutoka vyama mbalimbali wamepongeza kauli hiyo na kueleza kuwa amegusa hali halisi.

Akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Utoaji Elimu ya Sheria Dar es Salaam juzi, Mzee Mwinyi alisema, “Ili Mahakama iheshimike, haina budi kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote. Mahakama inatakiwa kudumisha nidhamu na kuzingatia maadili ya uhakimu na ujaji.”

Mzee Mwinyi alisema wakati akiwa Rais, alikuwa akipokea malalamiko ya watu wengi ambao walikuwa hawaridhiki na uamuzi wa Mahakama.

Akizungumzia kauli hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kauli ya Mzee Mwinyi ni kusisitiza haki katika chombo hicho cha sheria kwani huo ndiyo utaratibu, “Mahakama inatakiwa kuwa huru kwa mujibu wa sheria.”

Alisema uhuru wa Mahakama utaendelea kuheshimika endapo itaonekana inatenda haki kwa vitendo.

Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema Mzee Mwinyi amezungumza jambo lenye uzito na maana kubwa. Alisema baadhi ya uamuzi unaotolewa na Mahakama hautendi haki kama inavyotakiwa kuwa.

Lissu alisema mhimili huo unashindwa kutekeleza jukumu lake la kuisimamia Serikali ipasavyo.

Alisema katika nchi nyingi zilizoingia kwenye machafuko chanzo kikubwa kilikuwa mahakama kushindwa kutenda haki. “Mahakama inatakiwa itetee haki za wanyonge siyo kuibeba serikali, tutafika mahali watu watapoteza imani na vyombo vya sheria na hapo ndipo watakapojitosa kuchukua sheria mkononi,” alisema Lissu.

Hata hivyo, Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Onesmo Kyauke alitofautiana na Lissu akisema anaamini Mahakama za Tanzania ziko huru ikilinganishwa na nchi nyingine, licha ya kuwapo kwa changamoto kadhaa.

Pamoja na hayo, ili kuondoa mazingira kuwa Mahakama inaingiliwa, Dk Kyauke alishauri iwepo sheria itakayozuia watendaji wa ngazi za juu wa chombo hicho kupewa kazi serikalini.

“Si vizuri sana kwa majaji kuteuliwa kwenye nafasi serikalini mfano Msajili wa Vyama vya Siasa, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwani wakati mwingine inaweza kutengeneza mazingira kwa majaji wengine kufanya mambo ya kuifurahisha Serikali ili wapate nafasi hizo.

Suala la mishahara ya mahakimu nalo liangaliwe vizuri ili kusiwepo na mazingira ya rushwa na itengwe bajeti ya Mahakama sio kutegemea fedha kutoka serikalini. Ikiwezana hata asilimia tano ya bajeti kuu ielekezwe kwenye Mahakama.

Lakini Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CUF na Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya alisema kuwa mfumo wa Mahakama Tanzania unapaswa kubadilika.

Alisema kwa nafasi aliyonayo Mzee Mwinyi, huenda ameona vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya mahakama lakini viongozi wengine wanashindwa kuzungumzia.

“Mahakama inapaswa kuwa kimbilio la wananchi wanyonge ili waweze kupata haki, lakini mambo yamebadilika sasa rushwa inatumika kwa kiasi kikubwa kwenye utoaji wa maamuzi. Ukitaka kujua haya uwe unakutana na wananchi wa chini kabisa ndiyo utajua kuna kesi nyingi zinazoamuliwa kwa uonevu.”

Kauli ya kuonya Mahakama isiingiliwe pia ilitolewa na Wakili wa Crax Law Partners, Hamza Jabir, “Alichokisema Mzee Mwinyi ni kitu muhimu. Mahakama inatakiwa kuwa huru kama kuna mazingira ya kuingiliwa basi yaachwe mara moja maana itasababisha haki isitendeke.

Mahakama haitakiwi kuendeshwa kisiasa. Suala likishakuwa mahakamani halitakiwi kujadiliwa nje ya Mahakama na wasimamizi wa kesi wasiingiliwe.”

Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Danda Juju alisema mhimili huo umeshindwa kufanya kazi yake inavyostahili kutokana na kuingiliwa na Serikali.


Jumla ya tani 35,491 za chakula zinahitajika ili kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula na lishe kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili mwaka huu unaowakabili watu 1,186,028.

Taarifa hiyo ya serikali imetolewa bungeni leo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini huku akisisitiza kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini bado ni wa kuridhisha pamoja na kuwa baadhi ya maeneo yenye upungufu wa chakula.

Tizeba amesema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tathmini ya serikali iliyobaini kupungufu huo katika halmashauri 55 nchi nzima. 

Aidha amesema kuwa jumla ya watu 118,603 wasio na uwezo wa kupata chakula watahitaji tani 3,549 za chakula cha bei nafuu kwa haraka na tayari serikali imeanza kuchukua hatua za kushusha bei ili wananchi waweze kumudu bei zake.

Amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua na mtawanyiko usioridhisha katika maeneo mengi nchini athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na matarajio ya malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula huenda yasifikiwe, uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo utapungua, uwezekano wa kuongezeka kwa bei za baadhi ya mazao ya chakula upo, kupungua kwa mapato yatokanayo na ushuru wa mazao kwa baadhi ya halmashauri.

Athari nyingine ni pamoja na kuongezeka kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kutokana na uhaba wa malisho na maji na uwezekano wa kupungua kwa mapato yatokanayo na mazao ya kilimo yanayouzwa nje ya nchi, uwezekano wa kuwa na maeneo mengi yenye upungufu wa chakula na hivyo kuongezeka kwa kiwango cha utapia mlo.

Dkt.Tizeba amesema kuwa ili kukabiliana na athari za ukame tathmini imebainisha kuwa halmashauri za wilaya hizo 55 zinahitaji jumla ya tani 1,969 za mbegu bora za mahindi, mtama na mizizi inayokomaa kwa muda mfupi na kustahimili ukame na mbegu hizo zinahitajika ziwafikie mwezi Februari mwaka huu ili ziweze kupandwa katika msimu wa mwaka 2016 /2017 katika maeneo yanayoendelea kupata mvua wakati huu wa mwaka.


Nyalusi blog


 Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) na QT kwa mwaka 2016. Jumla ya watahiniwa 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 ya watahiniwa waliofanya mitihani kidato cha nne 2016 wamefaulu.

Wasichana waliofaulu ni 135,859 ambao ni swa na asilimia 67.06 wakati wavulana waliofaulu ni 142,424 sawa na asilimia 73.36.

Kwa mwaka 2015, watahiniwa waliofaulu walikuwa 272,947 sawa na asilimia 67.53. Ukilinganisha na matokeo ya mwaka huu, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.56. Idadi hii ni ya watainiwa wote, yaani watahiniwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea.

TEMBELEA www.necta.go.tz

Wanafunzi 10 Bora Kitaifa

     Alfred Shauri (Feza Boys)    Cynthia Nehemiah Mchechu (St. Francis Girls)    Erick Mamuya (Marian Boys)    Jigna Chavda (St. Mary Goreth)    Naomi Tundui (Maria Girls)    Victoria Chang’a (St. Francis Girls)    Brian Johnson (Marian Boys)    Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)    Ally Hassan Koti (ALCP Kilasara)    Emmanuel M. Kajege (Marian Boys)

Wasichana 10 Bora Kitaifa

    Cynthia Mchechu (St. Francis Girls)    Jigna Chavda (Mary Goreti)    Naomi Tundui (Maria Girls)    Victoria Chang’a (St. Francis Girls)    Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)    Christa Edward (St. Francis Girls)    Nelda John (Marian Girls)    Mariamu Shabani (Kifungilo Girls)    Beatrice Mwella (St. Mary’s Mazinde Juu)    Rachel Kisasa (Canossa)

Wavulana 10 Bora Kitaifa

    Alfred Shauri (Feza Boys)    Erick Mamuya (Marian Boys)    Brian Johnson (Marian Boys)    Ally Koti (ALCP Kilasara)    Emmanuel Kajege (Marian Boys)    John Ng’hwaya (Nyegezi Seminary)    Clever Yohana (Living Stone Boys)    Desderius Rugabandana (Morning Star)    Kennedy Boniface (Feza Boys)    Assad Msangi (Feza Boys)

Shule 10 Bora Kitaifa

    Feza Boys    St. Francis Girls    Kaizirege Junior    Marian Girls    Marian Boys    St. Aloysius Girls    Shamsiye Boys    Anwarite Girls    Kifungilo Girls    Thomas More Machrina

Shule 10 za Mwisho Kitaifa

    Kitonga    Nyeburu    Masaki    Mbopo    Mbondole    Somangila Day    Dahani    Ruponda    Makiba    Kidete


Na nyalusi blog

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.

Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali

Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara


Barack Obama amepumzika sasa baada ya kuitumikiaa Marekani kwa miaka minane kama Rais. Lakini, hiyo haimaanishi kuwa ametoka kwenye mzunguko wa fedha. Na tena, huenda akaanza kuingiza nyingi zaidi, asante kwa mikataba minono inayomuwinda kutoka kwa wachapishaji wa vitabu.

Yeye na mkewe Michelle, ni uamuzi wao tu, kukubali kusaini mikataba ya vitabu, yenye thamani ya kuanzia dola milioni 20 hadi 45. Fedha hizo, pamoja na matumizi mengine, zitamwezesha kugharamikia bili za ndege binafsi, sababu amewahi kudai kuwa hatopenda kusafiri na ndege za kawaida akistaafu.

Kwa mujibu wa New York Times, mawakala wa masuala ya vitabu wanadai kuwa Obama ana nafasi ya kuandika kitabu chenye thamani kubwa zaidi kuwahi kuandikwa na Rais yeyote.

Wengine wanadai kuwa Obama anaweza kuingiza zaidi ya dola milioni 12, na mkewe zaidi ya dola milioni 10.

Obama amewahi kuandika vitabu vitatu, “Dreams From My Father,” “The Audacity of Hope” na “Of Thee I Sing” ambavyo vimeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani na kumuingiza zaidi ya dola milioni 10.


Na nyalusiblog

SUALA la kuoa lipo tu licha ya kwamba wapo wanaochelewa kuingia kwenye maisha hayo wakihisi inaweza kusitisha furaha ya maisha yao. Nasema hivyo kwa kuwa najua wapo wanaoamini kuoa ama kuolewa ni kujiingiza kwenye matatizo.

Dhana hiyo haina mashiko kiviile, asikuambie mtu unapoingia kwenye ndoa na mtu anayekupenda na wewe unampenda kwa dhati, karaha hakuna licha ya kwamba kugombana kwa hapa na pale hakuwezi kukosekana.

Hata hivyo, nikiri tu kwamba, zipo ndoa ambazo ni ndoano. Yaani unakuta mtu kaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hakuwa amedhamiria, matokeo yake kadiri siku zinavyokwenda anahisi ameingia chaka na anaishia kuomba ndoa isiwepo.

Leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao ni majanga na ukijichanganya ukaingia nao kwenye maisha ya ndoa, utakiona cha mtemakuni.

10. Asiyeridhika na penzi unalompa
Wapo wanawake ambao wewe unaweza kujitahidi kumpatia mapenzi kadiri unavyoweza lakini yeye hatosheki. Anakuchukulia wewe ni dhaifu sana na wakati mwingine kuhisi yupo mwingine anayeweza kumpa zaidi ya kile unachompa, huyu ni tatizo.

9. Wivu kupindukia
Hatukatai, wivu ni muhimu sana kwenye suala la mapenzi lakini kuna ule wivu uliopindukia kiasi cha kuwa kero. Walio kwenye ndoa wananielewa namaanisha nini.

Kwa kifupi mtu mwenye mapenzi ya dhati na mwenziye lazima awe na wivu lakini ukiwa na ule wa kupinduki ni tatizo linaloweza kuitibua ndoa.

8. Anaona unamsaliti kila mara
Huku kunatokana na kutokujiamini tu. Ukioa mwanamke ambaye kila wakati unapokuwa mbali naye anahisi unamsaliti, huyo hakuamini na kamwe hamuwezi kudumu. Mara kadhaa mtakuwa mkigombana akihisi una mwingine kumbe hakuna ukweli katika hilo.

7. Anahisi amekosea kuwa na wewe
Wapo wanawake ambao wanapoingia kwenye ndoa baada ya muda wanahisi wamekosea kuolewa na mwanaume huyo. Unakuta mke wa mtu anahisi fulani ambaye zamani alikuwa kwenye uhusiano naye angekuwa sahihi zaidi baada ya kuona upungufu fulani kwa huyo aliyemuoa.

6. Yuko kimasilahi zaidi
Kuna wanawake ambao ukiwaoa wanakuwa na furaha na wewe ukiwa unazo tu, ukiishiwa wanaanza kununa na kuleta visirani vya hapa na pale. Hawa ni tatizo, mwanamke wa kweli ni yule anayeridhika kuwa na wewe kwenye shida na raha

5. Yuko tayari kuachana na wewe
Hivi hujawahi kumsikia mke wa mtu akimwambia mumewe; ‘Kama vipi tuachane, kwanza kwetu sijafukuzwa na nilikuwa nakula, nalala, navaa.” Mwanamke anayeweza kumtamkia mume wake maneno haya, huyo si mke na kamwe hawezi kukufanya uwe na furaha.

4. Hapendi ndugu zako
Waswahili wanasema ukipenda boga, penda na ua lake. Kama utatokea kuoa mwanamke ambaye anakupenda wewe tu lakini akija ndugu, rafiki au mtu mwingine wa karibu yako anabadilika, huyo ana matatizo kwani atakufanya utengwe na jamii yako.

3. Anajali mafanikio binafsi
Siku zote wawili waliotokea kupendana wakioana wanakuwa mwili mmoja hivyo lazima watakuwa wanawaza na kufanya maamuzi pamoja.

Ogopa sana mwanamke anayependa kutumia kipato chake kufanya mambo binafsi tena kwa siri. Kwa mfano kusaidia kwao, kujenga nyumba kwao, kuanzisha miradi yake bila kukushirikisha.

2. Eti akizaa utamzeesha
Hili kwa wale wanaopenda kuoa masistaduu. Wapo ambao wakitajiwa suala la kuzaa mara baada ya kuingia kwenye ndoa wanagoma wakidai eti watazeeshwa hivyo waachwe kwanza wale ujana. Wakati huo unaweza kukuta mwanaume anataka mtoto ili apate ile heshima, mke anagoma kwa sababu hiyo isiyo na msingi, hili ni tatizo.

1. Anataka awe na sauti
Mwanaume siku zote atabaki kuwa kiongozi wa familia lakini wapo baadhi ya wanawake hawataki kukubaliana katika hilo. Wengi wanalazimisha usawa na wengine wakitaka wao ndiyo wawe na sauti kuliko wanaume zao.


Rais wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais Conde anapokea uongozi kwa Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ni kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the Union). Mwenyekiti huyu huchaguliwa  na Marais wa Nchi wanachama wa AU ambaye hushika wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa zamu katika Kanda tano za bara la Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, na Afrika ya Kati).

Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002 ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza.


Rais wa Chad,  Idriss Deby (kushoto) akikabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Alpha Conde wa Guinea (kulia).

Kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Mwanza kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Mwanza, kimekamata watuhumiwa 14 wa uvuvi haramu, wakiwa na nyavu 1,660 za Makila, Makokoro matano ya Sangara, mitumbwi 8 na injini 7 za mitumbwi katika doria iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Afisa mfawidhi wa usimamizi wa raslimali za uvuvi kanda ya Mwanza Lameck Mongo amesema doria hiyo imefanyika katika kisiwa cha Makobe kilichomo ndani ya ziwa Victoria, ikiwa ni mwendelezo wa vita dhidi ya uvuvi haramu.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi wa polisi ACP Augustino Senga amesema watuhumiwa hao 14 waliokamatwa na zana hizo haramu za uvuvi watafikishwa mahakamani baada ya kuchukuliwa maelezo yao.

Msako dhidi ya uvuvi haramu unakuja wakati wavuvi wa mikoa ya Mara, Kagera, Simiyu na Mwanza wakiwa katika mgomo usiokuwa na kikomo kutokana na kupinga agizo la waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Dk. Charles Tizeba alilolitoa Januari 24 mwaka huu jijini Mwanza, la kuwataka kutumia nyavu zenye matundu 26, ambazo ni mwafaka kwa uvuvi endelevu badala ya nyavu zenye matundu 78 ambayo wanadai yamekuwa yakitumika tangu biashara ya usindikaji wa minofu ya Sangara viwandani ilipoanza mwanzoni mwa miaka ya 2000.


Nyalusi blog


Inasemekana wadada wana tabia tofauti katika mapenzi kulingana na maumbo ya miili yao,

Wasichana wafupi wanaongoza kwa wivu wa mapenzi na kuwajali wapenzi waoWasichana warefu huwa hawawajali wapenzi wao na hawaogopi mahusiano kuvunjia hawajui kubembeleza hata kidogoWasichana wenye DIMPOZ, MWANYA, MATEGE MBINUKO, MAHIPS NA KITHEMBE, hawa huongoza kwa kutokuwa WAAMINIFU katika mapenzi.Wasichana WANENE huongoza kwa MAPENZI YA KWELI yaani akipenda amependa kweliWasichana WEMBAMBA hawa huwa ni WABISHI sana na hawa wanaongoza kwa kutendwa!Wasichana wenye NGOZI NYEUSI wanaongoza kwa KUTOA MIMBA na kupenda wanaume warefu na weupeWasichana weupe wakiongoza kwa kuzalia nyumbani, na hawa weupe wengi wao huolewa wakiwa na watoto tayari huku wakipenda kuolewa na waarabu kuliko wanaume weusi.

Je kuna ukweli hapo?

Visit website

Author Name

{picture#YOUR_PROFILE_PICTURE_URL} YOUR_PROFILE_DESCRIPTION {facebook#https://fb.com/} {twitter#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {google#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL}

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.